Featured Kitaifa

MASHIRIKA YA UHTC NA UHIC WATOA VIFAA TIBA KWA AJILI YA KAMBI YA KUBWA YA MAGONJWA YA MASIKIO, PUA NA KOO (ENT)

Written by mzalendoeditor
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shiloo kushoto akipokea  vifaa tiba vilivyotolewa na mashirika ya  United Help for Tanzanian Children (UHTC) na United Help
For International Children (UHIC) vilivyotolewa kwa halmashauri ya Jiji la Tanga vyenye thamani ya milioni 12,533,000 kwa ajili ya kambi ya madaktari  bingwa  wa magonjwa ya masikio,pua na koo (ENT) itakayofanyika Agosti 10-15 mwaka huu.
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhamani Shiloo akizungumza kabla ya kupokea  vifaa hivyo kulia Mkurugenzi wa Shirika la United Help for Tanzaniani Children (UHTC) Regis Temba kushoto ni Mganga Mkuu wa Jiji la Tanga CMO

Mkurugenzi wa Shirika la United Help for Tanzaniani Children (UHTC) Regis Temba akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo

Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Mikanjuni Dkt Ummykulthum Kipanga akieleza namna watakavyotumia vifaa hivyo

Mganga Mkuu wa Jiji la Tanga (CMO) akizungumza

NA OSCAR ASSENGA, TANGA

MASHIRIKA ya United Help for Tanzanian Children (UHTC) na United Help For International Children (UHIC) wametoa msaada wa vifaa tiba kwa halmashauri ya Jiji la Tanga vyenye thamani ya milioni 12,533,000.

Msaada huo ulikabidhiwa kwa Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shiloo katika halfa iliyofanyika kwenye kituo cha Afya Mikanjuni ambavyo ni kwa ajili ya kambi kubwa ya matibabu kwa kutumia madaktari bingwa.

Akizungumza jana Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Mikanjuni Dkt Ummykulthum Kipanga alisema o alisema madaktari hao bingwa ni wa magonjwa ya masikio,pua na koo (ENT) itakayofanyika Agosti 10-15 mwaka huu.

Alisema kambi hiyo inatarajiwa kuwahudumia wagonjwa 300 (Screening) ambao kato yao hao takribani wagonjwa 100 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji

Aidha alisema kwa kulifanikisha kambi hiyo Halmashauri ya Jiji la Tanga iliomba wadau mbalimbali kutoa ushirikiano wa hali na mali kwa kuchangia mahitaji mbalimbali.

Awali akizungumza kabla ya kukabidhi msaada huo, Mkurugenzi wa Shirika la United Help for Tanzaniani Children (UHTC) Regis Temba alisema wameamua kukabidhi vifaa hivyo baada ya kupelekewa ombi na halmashauri ya Jiji la Tanga uwepo wa kambi hiyo.

Alisema hivyo wakaona wakabidhi vifaa hivyo kwa Mstahiki Meya kwa ajili ya maandalizi kwa ajili ya shughuli matibabu ya mfumo wa hewa ambao wanaamini itakuwa kambi hiyo itakuwa na tija kubwa.

Aidha alisema Shirika hilo limekuwa likitoa sapoti kubwa kwenye vituo vua Mikanjuni, Pongwe, Mafuriko na kila mwezi wana kawaida ya kuwapa dawa ili lengo likiwa kuhakikisha dawa kwa watoto chini ya miaka mitano wanapewa.

Alisema Shirika hilo pia limekuwa likitoa dawa za matibabu kila mwezi ambapo msaada huo unagharimu kiasi cha zaidi ya Sh. Milioni zaidi ya milioni 2 na mpaka sasa wametumia zaidi milioni 52.2 kuanzia mwaka 2020 mpaka Aprili mwaka huu na wameweza kutoa matibabu kwa watoto zaidi ya 24,231 wamekuwa wakinufaika nayo.

“Baada ya kupata maombi ya kutaka kusaidia kambi ya itakayoanza Agosti 10-15 kutokana na kwamba jami inahaingaika sana na shirika hilo ni kuhakikisha watoto wanakuwa na afya bora kituo kiliomba msaada na Shirika UHTC tuliona tutoe msaada huo”Alisema

Awali akizungumza mara baada ya kupokea vifaa hivyo Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shiloo alilishukuru shirika hilo kwa kuamua kutoa msaada huo ambaop utakwenda kuwa chachu wakati wa kambi hiyo huku akitoa wito kwamba vifaa hivyo vitumike kwenye malengo yaliyokusudiwa na sio vyenginevyo.

“Kwa kweli niwashukuru kwa msaada huu ambao mmetupatia kwa ajili ya kambi yetu lakinio niwaombe wadau wengine nao waona umuhimu wa kutusaidia katika kufanikisha hilo”Alisema Mstahiki Meya huyo.

Hata hivyo aliwapongeza watumishi wa vituo vya afya kwa kazi nzuri wanayoifanya huku akieleza kwa niaba baraza la madiwani sasa hivi Tanga ina kaa kwenye mstari na tunakwenda vizuri.

“Niwahakikishie kwamba Baraza la Madiwani lipo pamoja nanyi lakini niwaambie msiangalie mmeletewa vifaa kutumia mapato ya papo kwa papo badala yake mtoke nje ya box muangalie wafadhili na wadau wengine nisisitize vifaa hivyo vitumike kwenye matumizi yaliyokusudiwa na sio vyenginevyo na viwekwe stooo vizuri na view maalumu kwa ajili ya kambi na acheni kuvitumia kabla ya kambi kuanza”Alisema

About the author

mzalendoeditor