Featured Kitaifa

RAIS DKT. MWINYI ATOA MKONO WA POLE

Written by mzalendoeditor

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) leo amefika Nyumbani kwa Mfanyakazi wake kutoa mkono wa pole baada ya kifo cha Baba Mzazi wa Mfanyakazi huyo huko nyumbani kwao Dole,Ndunduke Wilaya ya Magharibi”A” Mkoa wa Mjini Magharibi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akisalimiana na wanafamilia wa Marehemu Bw.Mohamed Ali Juma mume wa Mbunge wa Jimbo la Bububu Mhe.Mwantakaje Haji Juma alipofika  Nyumbani kwao Bububu Kijichi Wilaya ya Magharibi”A” Mkoa wa Mjini Magharibi kutoa mkono wa pole.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati)  alipofika  Nyumbani kwa  Mbunge wa Jimbo la Bububu Mhe.Mwantakaje Haji Juma (wa pili kulia) leo  kutoa Mkono wa pole baada ya kufiliwa na mume wake Marehemu  Mohamed Ali Juma,  Kijichi Wilaya ya Magharibi”A” Mkoa wa Mjini Magharibi .

Picha na Ikulu.  

About the author

mzalendoeditor