Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasha Lori lenye thamani ya shilingi milioni 110 baada ya kulikabidhi kwa kikundi cha vijana wa kijiji cha Mandawa wilayani Ruangwa ili walitumie katika mradi wao wa kufyatua matofali. Alikuwa katika ziara ya kakazi wilayani humo,
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua lori alilolikabidhi kwa kikundi cha vijana cha Mandawa wilayani Ruangwa akiwa katika ziara ya kikazi wilayani humo, Julai 8, 2022. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Frank Chonya.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Mandawa wilayani Ruangwa akiwa katika ziara ya kikazi wilayani humo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mashine ya kufyatua matofali aliyoikabidhi kwa kikundi cha vijana cha kijiji cha Mandawa wilayani Ruangwa Julai 8, 2022. Shilingi Milioni 25 za kununua mashine hiyo zimetolewa kwa mkopo kwa kikundi hicho na halmashauri ya wilaya Rungwa. Wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack na watatu kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya ya Ruangwa, Frank Chonya. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)