Featured Kitaifa

KAMATI YA BUNGE YA BAJETI YARIDHISHWA NA USIMAMIZI WA FEDHA ZA UVIKO-19 KATIKA UJENZI WA JENGO LA UFUNDI TOWER

Written by mzalendoeditor
Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya bajeti Daniel Sillo akiongea na waandishi wa habari wakati walipotembelea jengo la ufundi Tower.
 Kamati ya Bunge ya bajeti wakimsikiliza maelezo kutoka kwa Mhandisi wa mradi huo Faraji Mfinanga ambaye pia ni meneja wa kitengo cha ufundi katika chuo hicho.
Naibu Waziri wa Elimu, sayansi na teknolojia Omary Kipanga akiongea wakati kamati ya Bunge ya bajeti ilipotembelea jengo la ufundi Tower katika chuo cha ufundi Arusha.
Mkuu wa chuo cha ufundi Arusha Dkt Musa Chacha akiongea wakati kamati ya Bunge ya bajeti ilipotembelea jengo la ufundi Tower katika chuo hicho.
Muonekano wa jengo la ufundi Tower lililokamilika kwa asilimia 95 katika chuo cha ufundi Arusha.
KAMATI ya Bunge ya bajeti wakiangalia mchoro wa ramani ya ujenzi wa jengo la ufundi Tower katika chuo cha ufundi Arusha.
………………………………………
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti  imeridhishwa na usimamizi wa fedha za UVIKO-19 katika ujenzi wa madarasa,maabara na ofisi katika chuo cha Ufundi Arusha(ATC) maarifu kwa jina la Ufundi Tower  ambayo imekamilika kwa asilimia zaidi ya 90.
Akiongea wakati walipotembelea jengo hilo mwenyekiti wa kamati hiyo Daniel Sillo alisema kuwa wamejionea jinsi Flfedha za UVIKO-19 zilivyofanya kazi kubwa na kumpungeza Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia Hassan Whiteside kwa kuhakikisha vyou vya ufundi vinakuwa na miundombinu inayokidhi viwango vya utoaji elimu ili kusaidia jamii kuongeza ujuzi na kuleta tija.
Alisema kuwa jengo hilo lililogharimu bilioni 2.2  zimesaidia ujenzi wa madarasa nane yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 880 kwa wakati mmoja,maabara sita zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 270 kwa wakati mmoja ikiwemo ofisi 26 zenye uwezo wa kuchukua watumishi 104.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Elimu, sayansi na teknolojia Omary Kipanga aliishukuru serikali kwa kuboresha vyuo mbalimbali ikiwemo kujenga vyuo vinne vya ufundi katika maeneo ambayo hayakuwa na vyuo ambapo bilioni 20 zimepelekwa kwaajili ya kujenga vyuo vinne katika mikoa ya Rukwa,Geita,Njombe na Simiu
“ katika chuo hiki Wizara ya Elimu pia imetoa milioni 523 kwaajili ya kununua samani za majengo  lakini pia  mtaala mpya wa elimu utawezesha na  kuwasaidia wanafunzi kupewa ujuzi wa vitu mbalimbali vyenye bunifu zenye tija kwaajili ya kuleta tija kwa wananchi na kuongeza ajira, Alisema 
Naye Mkuu wa chuo cha ufundi Arusha Dkt Musa Chacha alishukuru serikali kwa kuhakikisha inaongeza tija kwa vyuo vya ufundi huku akisisitiza kuwa kukamilika kwa jengo hilo kutapunguza msongamano wa wanafunzi katika madarasa na maabara 
Alieleza kuwa pia itapunguza msongamano wa wanataaluma katika ofisi chache pamoja na  msongamano wa ratiba za masomo kutokana na uchache wa madarasa na maabara ikiwemo kuondoa baadhi ya vipindi kufundishwa muda wa jioni sana na hata nyakati za usiku.
Nao baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo  Halima Mdee aliipongeza chuo hicho kwa kuongeza idadi kubwa ya wasichana ambapo katika mwaka wa masomo 2021/22 chuo kina jumla ya wanafunzi 4,693 ikilinganishwa na wanafunzi 2,017 waliokuwepo mwaka 2015/16 ikiwa ni ongezeko la asilimia 132.

About the author

mzalendoeditor