Featured Kitaifa

KATAMBI AKABIDHI VIFAA MTAJI KWA VIKUNDI VYA VIJANA VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 371

Written by mzalendoeditor

Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye ulemavu, Patrobas Katambi,akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa mtaji kwa vikundi vya vijana na watu wenye ulemavu  leo Julai 1,2022 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye ulemavu,Prof.Jamal Katundu,,akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa mtaji kwa vikundi vya vijana na watu wenye ulemavu  leo Julai 1,2022 jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakifatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye ulemavu, Patrobas Katambi (hayupo pichani), wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa mtaji kwa vikundi vya vijana na watu wenye ulemavu  leo Julai 1,2022 jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye ulemavu, Patrobas Katambi,akimkabidhi Kaimu Katibu Mkuu TAMISEMI ambaye pia ni Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Serikali za Mitaa kutoka TAMISEMI, Humphrey Mniachi, vifaa mtaji kwa vikundi vya vijana na watu wenye ulemavu  leo Julai 1,2022 jijini Dodoma.

Kaimu Katibu Mkuu TAMISEMI ambaye pia ni Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Serikali za Mitaa kutoka TAMISEMI, Humphrey Mniachi, akigawa vifaa mtaji kwa vikundi vya vijana na watu wenye ulemavu kwa wawakilishi wa vijana leo Julai 1,2022 jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye ulemavu, Patrobas Katambi,akiwa katika picha na vijana mara baada ya kukabidhi vifaa mtaji kwa vikundi vya vijana na watu wenye ulemavu  leo Julai 1,2022 jijini Dodoma.

Kaimu Katibu Mkuu TAMISEMI ambaye pia ni Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Serikali za Mitaa kutoka TAMISEMI, Humphrey Mniachi,akitoa pongezi kwa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye ulemavu kwa kukabidhi vifaa mtaji kwa vikundi vya vijana na watu wenye ulemavu  leo Julai 1,2022 jijini Dodoma.

MWAKILISHI wa vikundi vya vijana Gladis Jamal,akiishukuru Serikali ya awamu ya 6 kwa kuwapatia vifaa hivyo ambavyo vitaenda kuwasaidia kujiajiri na kujikwamua kiuchumi.

……………………………………..

Na Alex Sonna-DODOMA

SERIKALI imekabidhi vifaa mtaji kwa vikundi vya vijana na watu wenye ulemavu vyenye  thamani ya zaidi ya shilingi milioni 371 kwa vikundi 174 na vitapelekwa katika Mikoa 26  vitakavyokwenda kuwanufaisha vijana zaidi ya 1400 kupitia vikundi vyao .

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo leo Julai 1,2022 jijini Dodoma Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye ulemavu, Patrobas Katambi,amesema kuwa  vifaa hivyo ni pamoja na vifaa vya kushonea (cherehani),Vifaa vya uungaji vyuma pamoja na Vifaa vya uchomeleaji aluminium.

Katambia amesema kuwa  ofisi hiyo imeamua kuanzisha utaratibu wa kugawa vifaa mtaji ambapo kwa mwaka huu zimenunuliwa cherehani 400, seti 75 za mashine za uchomeleaji na uungaji vyuma pamoja na seti 70 za mashine za kutengeneza vifaa vya aluminum.

“Vifaa hivi vimegharimu Sh.Milioni 371 na vitagaiwa kwa vijana hao ili kuvitumia kuzalisha zaidi lakini ni mkakati wao wa kujiajiri, Ofisi yetu imekuwa ikitekeleza program mbalimbali za vijana kwa kushirikiana na wadau mbalimbali,”amesema Katambi.

Katambi amesema kuwa  Ofisi hiyo ilishirikiana na TAMISEMI kuweka vigezo vya kuwapata vijana watakaopewa vifaa hivyo ikiwamo wenye ulemavu, kujiunga kikundi na vikundi vinavyorejesha mikopo kwa wakati kwenye Halmashauri zao.

Aidha amewataka vijana watakaopata fursa hiyo wakapate ushauri kutoka kwa wataalamu ili shughuli zao zikawe na tija sambamba nakuzitaka halmashauri kutoa tenda kwa vikundi vya vijana ili kuwakwamua kiuchumi na kupata faida itakayowawezesha kurejesha mikopo hiyo

“Kuliko kuwapa vijana fedha bila kuwapa elimu TAMISEMI na ofisi ya Waziri Mkuu itabidi itabidi tujipange ili kwenda kutoa elimu zaidi ili fedha itakayorejeshwa iwapatie watu wengine”

Awali, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Prof.Jamal Katundu,amesema lengo la kutoa vifaa hivyo ni kuwezesha mchakato wa kutoa ajira kwa vijana.

”Vifaa hivyo ni jitihada za serikali katika kuimarisha vikundi ambavyo vimekuwa vikinufaika na mikopo ya Halmashauri”amesema Prof.Katundu

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Serikali za Mitaa kutoka TAMISEMI, Humphrey Mniachi, amesema kuwa ugawaji wa vifaa unatekeleza dhana ya ugatuaji madaraka.

About the author

mzalendoeditor