Featured Kitaifa

MAOMBI MADOGO YA KUMUONDOA HATIANI WAKILI PETER MADELEKA YAHAIRISHWA, HAKIMU ASISITIZA UZINGATIAJI WA MUDA

Written by mzalendoeditor

WAKILI Peter Michael Madeleka akiongea na waandishi wa habari nje ya mahakama.

……………………………….
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
 Maombi madogo ya jinai namba 1/2022 yaliyoletwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na Peter Michael Madeleka dhidi ya Jamhuri ya kumuondoa hatiani kutokana na hukumu ya kesi ya ujuhumu uchumi namba 40/2020 imehairishwa hadi Julai 13,2022.
Akitoa maamuzi madogo ya kuhairsha shauri hilo kutokana na wakili mwandamizi wa serikali kutofika kwa wakati pamoja na kutoa maombi ya kuhairishwa kwa kesi hiyo, Hakimu Herith Mhenga alisema kuwa amehairisha kesi hadi Julia 13, 2022 na kutoa onyo kuwa iwe mara ya mwisho pamoja na kisisitiza kuzingatia muda.
“Mwombaji ameomba kesi hii isiahirishwe na kuiomba mahakama iendeelee na usikilizwaji nimenotice vifungu ambavyo mwombaji amevitaja katika Katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ambavyo vinaitaka mahakama isicheleweshe haki lakini Kimsingi kwa kesi za namna hii pande zote mbili ni vizuri wapewe haki ya kusikilizwa, sina sababu yoyote ya kutoa shaka sababu za wakili Akisa lakini kesi hii tumeipanga muda mrefu ilipaswa wote muwe tayari, sababu ya kusema tuu kwamba ulikuwa na kesi nyingine haitoshi kusema tusiendelee na kesi,”Alisema Hakimu Herith Mhenga.
“Lakini nimeangalia kwa upande mwingine interest of Justice iko safe, hatuwezi kulazimisha kusikiliza kesi hii kama hamjajipanga ili muweze kusikilizwa kwa ufasaha kwahiyo tunakubali kuhairishwa lakini iwe hairisho la mwisho na wakati mwingine tukiwa tunapanga kesi mzingatie muda isiwe kuna kesi zinasikilizwa na nyingine hazisikilizwi kwahiyo kwa mrengo huu tukipanga tarehe iwe kwa kesi hii au nyingine isikilizwe kwa tarehe tuliyopanga sio kwasababu chache kwani mahakama na yenyewe inajipanga kusikiliza kesi,” Alisema.
Awali akiongea katika mahakama hiyo wakili mwandamizi wa serikali Akisa Mhando alisema hayupo tayari katika usikilizwaji wa kesi hivyo kutokana na ana majukumu mengine aliyopangiwa ambayo yamepelekea kutopata muda wa kujitosheleza kujiandaa kwaajili ya kesi ndio maana ameomba ihairishwe mpaka siku nyingine.
Kwa upande wake muombaji wa kesi hiyo Peter Michael Madeleka akiongea ndani ya mahakama alisema kuwa sababu zote alizozisema hazina msingi kisheria na kunukuu ibara 107 A kubwa ibara ndogo ya pili B ya Katiba ya Jamuhuri ambayo alinukuu kwa kusema “katika kutekeleza wajibu wa kutoa haki mahakama zote nchini hazitachelewesha haki kwa sababu zozote” ambapo wakili wa serikali hajatoa uthibitisho wowote wa kisheria unaunga mkono sababu zake za kutoendelea kwa shauri hilo leo.
“Kesi hii ina umuhimu sawa na kesi zote zilizopo hapa mahakamani kwahiyo kitendo cha kuja kuambiwa siku ya kesi kuwa hawezi kuhudhuria ni dharau kwa mahakama, Kwa heshima zote na ili mahakama isionekane inafanya kazi kwa kutegemea upande fulani utaamua nini naomba tuendelee na shauri hili,” Alisema muombaji.
Akijitetea wakili mwandamizi wa serikali Akisa Mhando alisema hana haja ya kunidanganya mahaka ni kweli alikuwa kwenye kesi ya economic namba 4/2022 na 3/2022 na kesi zote zilikuwa zimepangwa muda mmoja ndio maana akashindwa kuhudhuria hiyo.
Aidha akiongea nje ya mahakama na waandishi wa habari muombaji Peter Michael Madeleka ambaye ni Wakili alisema amekuja mahakamani hapo kwaajili ya usikilizwaji wa kesi ya maombi namba 1/2022 ambapo katika maombi hayo alikuwa anaomba mahakama ya hakimu mkazi Arusha iweze kutengua amri iliyotoa ya kumtia hatiani kwa kosa la uhujumu uchumi kwa njia ya pre- bagein ambayo ilifanyika April 24,2021.
“Nimekuja mahakamani kwasababu utaratibu uliotumika kufanya pre bagein ile ambayo hatimaye ilipelekea mimi kutiwa hatiani na mahakama hii haukufuata sheria, haukuzingatia sheria na ulikuwa kabisa ni kinyume na haki jinai na sababu mojawapo ni aliyepokea pesa za pre bagein kwenye shauri hilo kisheria kwa mujibu wa kanuni ya 21 kanuni ndogo ya tatu (a) hakutakiwa kupokea hizo hela,” Alisema Wakili Madeleka.
Alifafanua kuwa jambo lingine analolilalamikia ambalo ndio msingi wa maombi yake ili mahakama iweze kutengua ni kwamba kosa alilohukumiwa nalo halikuwa kosa la uhujumu uchumi aliloshtakiwa nalo tangu awali bali ni kosa ambalo aliliona kwa mara ya kwanza siku ambayo alipelekwa mahakamani lakini pia alimlipa pesa DPP machi 30,2021 mwezi mzima kabla hawajafanya makubaliano yaliyofanyika mahakamani alilipa akiwa Gerezani na hakuwa na namna nyingine yoyote
“Sasa kilichojiri leo mahakamani kinasikitisha sana mimi kama mleta maombi nilikuwa nipo tayari kusikiliza shauri hili kama ilivyokuwa imepangwa lakini tumekaa mahakamani baada ya kuitwa kwenye chumba cha mahakama tangu asubuhi tukaja kuingia kwenye shauri saa saba mchana kwasababu mawakili wa serikali walikuwa hawaonekani na hata walipo onekana yalikuwa ni kinyume na amri ya mahakama ya kulitaka shauri hili leo,” Alieleza.

About the author

mzalendoeditor