Featured Kitaifa

BODI YA NNE YA MAJI YA TAIFA YAZINDULIWA RASMI JIJINI DODOMA

Written by mzalendoeditor
WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso,akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa  Bodi ya nne ya Maji ya Taifa iliyofanyika jijini Dodoma . 
Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi,akizungumza wakati wa uzinduzi wa  Bodi ya nne ya Maji ya Taifa hafla iliyofanyika jijini Dodoma . 
SEHEMU ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Maji Jumaa Aweso (hayupo pichani)  wakati wa hafla ya uzinduzi wa  Bodi ya nne ya Maji ya Taifa iliyofanyika jijini Dodoma . 
Mkurugenzi wa Rasilimali za maji kutoka Wizara ya Maji, Dk George Lugomela,akizungumza wakati wa uzinduzi wa  Bodi ya nne ya Maji ya Taifa hafla iliyofanyika jijini Dodoma . 
WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua Bodi ya nne ya Maji ya Taifa iliyofanyika jijini Dodoma . 
……………………………………….

Na Eva Godwin-DODOMA

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso,amezindua Bodi ya nne ya Maji ya Taifa huku akiitaka bodi hiyo kuongeza wigo wa kupeleka huduma ya maji kwa wananchi.
 
Hayo ameyasema jijini Dodoma wakati akizindua Bodi ya nne ya Maji ya Taifa 
Waziri Aweso,amewahakikishia Watanzania hatakuwa kikwanzo katika kuhakikisha idara ya maji inafanya vizuri katika suala zima la Maji nchini, huku akiwashukuru Wajumbe wa bodi ya Taifa iliyopita kwa utendaji kazi wao.

Pia amewaomba viongozi wa bodi kuwa wabunifu na kuwa washirikishi katika kufanikisha majukumu yao ya kutunza rasilimali Maji.

“Tunawaakikishia Watanzania wote katika Suala zima la Maji hamtoteseka,wala hatutakuwa kikwazo kwenu na ushirikiano wenu kwetu ni Muhimu ili tuendelea kufanya vizuri kama bodi iliyopita”,amesema

“Najua Bodi hii ya Nne mtaongeza ubunifu zaidi ili kazi ziende sawa kama tulivyopanga,nyie ndio mtafanya tuone manufaa makubwa katika bodi hii na baada ya takwimu ya sensa kupatikana ya mwaka 2022 najua kutakuwa na mfumo mpya wa ugawaji wa maji Ili kusaidia watu kupata maji kwa urahisi”.Amesema Aweso

Waziri Aweso amesema  kuwa sasa wanajivunia mafanikio makubwa ya Wizara hiyo ikiwemo kwa mara ya kwanza bajeti ya Wizara hiyo kupitishwa kwa asilimia 100.
“Ni aibu na fedheha kuwa Wizara ya lawama lakini sasa tuna mengi ya kujivunia kwani hata ile miradi chechefu tumefanikiwa kukwamua miradi 126,” amesema
 
Aidha Aweso ameziagiza Bodi za mabonde kuhakikisha wanaendelea na utendaji kazi wao vizuri ili kuongeza tija katika usimamizi wa raslimali za maji.
“Bodi za maji za mabonde kufanya udhibiti uchafuzi wa vyanzo vya maji na mchakato wa sheria uko mbioni kukamilika,” amesema.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi,amewaomba Wakurugenzi wa bodi hiyo walioteuliwa na Waziri Aweso wakasimamie majukumu yao ya utekelezaji katika kazi.

“Naamini kuwa Wasifu wenu ndio umemshawishi Mh.Waziri Aweso kuwateua kati ya wengi walio kuwa kwenye kinyang’anyiro hiko”,amesema

“Tunaamini mnaenda kuifanya kazi iliyobora kama alivyosema Mh.Waziri mkawe wabunifu,na msisite kuomba ushauri kwa bodi iliyopita,kazi nzuri ni ushirikiano kwaio msisite kuomba ushirikiano kwa bodi ya Tatu”.Amesema Mahundi.

Naye Mkurugenzi wa Rasilimali za maji kutoka Wizara ya Maji, Dk George Lugomela amesema kuwa Bodi hiyo iliteuliwa rasmi Aprili 2021 na Bodi inaundwa  na Mwenyekiti na wajumbe 11.
Dk.Lugomela amesema kuwa kazi kuu kwa bodi hiyo ni kumshauri Waziri juu ya masuala yanayohusu raslimali za maji na utatuzi wa migogoro wenye sura ya Kitaifa na kimataifa.
“Bodi hii pamoja na jukumu la kumshauri Waziri ipewe meno ya kudhibiti shughuli za mabonde ya maji , ipewe meno kidogo isiwe ya kushauri tu,” amesema .

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Nne ya Maji ya Taifa Eng.Mbogo Futakamba ameithibitishia serikali kuwa watafanya kazi kwa juhudi,weledi na Maarifa.

“Tupo pamoja na wewe Mh.Waziri tunahakikisha suala la Maji litatatuliwa kwa Wananchi wote kwasababu maji yanagusa kilakitu

“Usalama wa Elimu ni Maji,Usalama wa chakula ni Maji,Usalama wa Nishati ni Maji,Usalama wa Mazingira ni Maji na Maji ni usalama wa Maisha ya kila Mtu”.Amesema Futakamba

 

About the author

mzalendoeditor