Featured Kitaifa

MWALIMU AJIFUNGUA MAPACHA WANNE TUNDURU

Written by mzalendoeditor

 Mkuu wa wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro wa pili kulia akiwa amemshika mototo mmoja kati ya watoto mapacha wanne wa Mwalimu  wa shule ya msingi Wenje kata ya Nalasi wilayani humo Judith Chawe,wa kwanza kulia Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Tunduru Ombeni Hingi.

Mkuu wa wilaya ya Tunduru na Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo Julius Mtatiro wa tatu kushoto na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo wakiwa wameshika watoto mapacha wa Mwalimu wa shule  ya msingi Wenye wilayani humo Judith Chawe wa kwanza kulia na mumewe Hamis Hamza Shaibu.

………………………………..

Na Muhidin Amri,
Tunduru

MWALIMU wa shule ya msingi Wenje kata ya Nalasi wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Judith Chawe(29), amejifungua watoto wanne katika Hospitali ya Misheni Mbesa wilayani humo.

Mwalimu Judith alisema kuwa,watoto aliojifungua wenye jinsia ya kiume ni wawili na wa kike wawili na alifungua kwa njia ya kawaida na wanaendele  vizuri na kuongeza kuwa huo ni uzazi wake wa pili.

“Kwanza namshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha kujifungua salama,lakini kutokana na mahitaji makubwa ya watoto wangu  nawaomba wasamaria wema na Watanzania wenzangu wenye mapenzi mema wanisaidie  mahitaji mbalimbali kama fedha  na maziwa ili niweze kuwalea  hawa watoto”alisema Mwalimu Chawe.

Alisema,wakati anahudhuria kliniki Madaktari walimweleza kuwa ana watoto watatu tumboni,lakini kumbe walikuwa wanne  na kumshukuru Mungu kwa kumwezesha kupata watoto  hao na ameruhusiwa kurudi nyumbani.

Baba mzazi wa watoto hao Hamis Shaibu amemshukuru Mungu kwa kumwezesha kupata watoto wanne kwa mkupuo,hata hivyo ameiomba jamii iweze kuwasaidia  kwa hali na mali  mahitaji ya watoto hao.

Mkuu wa wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro amefika nyumbani kwa Mwalimu huyo ili kumjulia hali  na kuwaona watoto hao ambapo amewaomba Watanzania wenye mapenzi mema kumsaidia Mwalimu Judith ili aweze kuhudumia watoto hao wanaohitaji  gharama kubwa.

Mtatiro alisema,watoto hao wanahitaji msaada na huduma ya karibu kwa sababu maziwa ya mama peke yake hayatoshelezi kuwahudumia watoto hao wote wanne.

Alisema,serikali itakuwa bega kwa bega na Mwalimu huyo ili  uona maendeleo ya afya yake na watoto hao na amemwagiza Kai u Mkurugenzi wa Halmashauri  ya Tunduru Ombeni Hingi, kuhakikisha Halmashauri inampatia gari Mwalimu huyo kila atakapohitaji  kwenda Hospitali kwa ajili ya uchunguzi wa afya ya Mwalimu huyo na watoto wake.

Alisema,kazi ya malezi ya watoto wanne ni kubwa kwa hiyo lazima Serikali na jamii kums idia Mwalimu Judith katika malezi ya watoto hao waendele  kukua vizuri na kuwa na afya njema.

Awali Afisa Tarafa wa Nalasi  Salum Kijumu alisema, baada ya kupata taarifa ya Mwalimu Ju ith kujifungua watoto wanne wameanza utaratibu wa kumchan ia  fedha kutoka kwa watumishi wanaofanya kazi katika Tarafa hiyo ili ziweze kusaidia mahitaji ya watoto hao.

About the author

mzalendoeditor