Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza Askofu Wolfgang John Pisa baada ya askofu huyo kusimikwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi katika ibada iiyofanyika kwenye uwanja wa Ilulu mjini Lindi,
Askofu Wolfgang John Pisa akiwa amelala kifudifudi katika Ibada ya kusimikwa kwake kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi iliyofanyika kwenye uwanja wa Ilulu mjini Lindi, Juni 26, 2022. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alishiriki katika Ibada hiyo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na baadhi ya viongozi walioshiriki katika Ibada ya kumsimika Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi Wolfgang John Pisa wakifuatilia ibada hiyo iliyofanyika kwenye uwanja wa Ilulu mjini Lindi, Juni 26, 2022. Kushoto ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack.
Baadhi ya washiriki wa Ibada ya kusimikwa Askofu Wolfgang John Pisa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi wakifauatilia Ibada hiyo kwenye uwanja wa Ilulu mjini Lindi,
Baadhi ya Mapadri walioshiriki katika Ibada ya kusimikwa Askofu Wolfgang John Pisa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi wakifauatilia Ibada hiyo kwenye uwanja wa Ilulu mjini Lindi
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)