KATIBU
Mkuu wa Chama cha Aliance Demokratc Change (ADC) Doyo Hassan Doyo
akizungumza na wananchi wa Kata ya Mabanda Jimbo la Handeni mjini
KATIBU
Mkuu wa Chama cha Aliance Demokratc Change (ADC) Doyo Hassan Doyo kulia
akigaiawa kadi kwa wanachama wapya waliojiunga na chama hicho mara
baada ya kuzindua tawi hilo
KATIBU
Mkuu wa Chama cha Aliance Demokratc Change (ADC) Doyo Hassan Doyo kulia
akigaiawa kadi kwa wanachama wapya waliojiunga na chama hicho mara
baada ya kuzindua tawi hilo
KATIBU
Mkuu wa Chama cha Aliance Demokratc Change (ADC) Doyo Hassan Doyo kulia
akigaiawa kadi kwa wanachama wapya waliojiunga na chama hicho mara
baada ya kuzindua tawi hilo
KATIBU
Mkuu wa Chama cha Aliance Demokratc Change (ADC) Doyo Hassan Doyo
amesema suala la CCM kuzungumzia mchakato wa Katiba mpya kwamba
imeridhia na wanasubiri Serikali ione namna gani linafufuliwa
wamelipokea kwa mikono miwili.
Doyo aliyasema hayo leo mjini
Handeni wakati akifungua Tawi Mtaa wa Mabanda Kata ya Mabanda Jimbo la
Handeni Mjini na kufanikiwa kupata wanachama zaidi ya 60 ambao
walichukua kadi ya ADC huku akiwashukuru wananchi kwa kukiunga mkono
chama hicho .
Alisema hivi sasa wanasubiri
Serikali iweze kuona namna gani jambo hilo linafufuliwa ili mchakato
uanze huku akieleze wamelipokea kwa furaha japokuwa hawaamini kwamba CCM
wana nia thabiti ya kujenga mifumo ya katiba ambayo watanzania
wanaihitaji.
Alisema kutokana na wasiwasi huo wanaitaka Serikali
ya CCM iweze kutoa tamko la haraka la kukubali huo mfumo na kwamba
unaanza lini na mchakato wake utakuwaje kutokana na kwamba ni suala
rahisi sana .
“Kwani sheria ya mabadiliko ya katiba imeshatungwa
hivyo ni kuifufua tu na bunge bado linakaa na tunaamini kama Serikali
ipo makini na suala ka katiba mpya na CCM imebariki hivyo itoa tamko
haraka ni lini mchakato wa katiba mpya utaanza”Alisema Katibu Mkuu huyo.
Hata hivyo alisema suala la katiba mpya kwa watanzania ni
muhimu sana na ndio maana wamekuwa wakilipigia kelele mara kwa mara ili
kuhakikisha inapatikana.
Katika hatua nyengina Katibu huyo Mkuu
aliwataka wananchi wa Kata hiyo kuhakikisha wanajitokea ,kwa wingi
kuhesabiwa wakati wa zoezi la Sensa ya watu na Makazi linatalofanyika
mwezi Agosti mwaka huu hapa nchini kutokana na kwamba ni tukio muhimu
kwa nchi.