Burudani Featured

BALOZI WA UTALII LYDIA AMUUNGA MKONO RAIS SAMIA KWA KUANZISHA MBIO ZA MARANGU NATURE WALK RIDE&RUN

Written by mzalendoeditor

BALOZI wa Utalii nchini
Lydia Lukaba akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza mbio za Marangu Nature Walk Ride&Run
zenye lengo la kutangaza utalii wa ndani kulia ni Afisa Uhifadhi kutoka Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro Vitus Mgaya

BALOZI
wa Utalii nchini
Lydia Lukaba akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza mbio
za Marangu Nature Walk Ride&Run
zenye lengo la kutangaza utalii wa ndani kulia ni Afisa Uhifadhi kutoka
Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro Vitus Mgaya na  kushoto ni Fredy Moshi
kutoka Ndoro
Water Fall

Afisa
Uhifadhi kutoka Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro Vitus Mgaya akizungumza
na waandishi wa habari kushoto ni Fredy Moshi kutoka Ndoro
Water Fall

Fredy Moshi kutoka Ndoro
Water Fall akizungumza

Meneja wa Hotel
ya Hosea Inn Marangu Dues Masawe akizungumza

NA OSCAR ASSENGA,MOSHI.

BALOZI wa Utalii nchini
Lydia Lukaba ameunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu za kutangaza
utalii nchini kwa kuanzisha mbio za Marangu Nature Walk Ride&Run
zenye lengo la kutangaza utalii wa ndani

Akizungumza na
waandishi wa habari mjini Marangu Balozi Lydia alisema licha ya
kuzitumia kutangaza utalii wa ndani lakini pia watachangia taulo za Kike
kwa ajili ya watoto wa kike ambao hawana uwezo kwa kupatiwa msaada huo.

Alisema mbio hizo ambazo zitakwenda sambamba na matembezi
zitakuwa endelevu na zitafanyika Julai 10 mwaka huu na zitaanzia Marangu
Mtoni yatakuwa ya kilomita 50,21 mara mbili na kilomita 40 za baiskeli
na Kilomita 5.

Balozi Lydia ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni
ya Conservation Marathon alisema mbio hizo zitapita eneo la Kinukamori
Water fall na kilomita 10 zitakwenda Ndoro Water falls wakati zile za
Kilomoita 21 zitaanza kinapa na kwenda Mandara na kumalizika Marangu
mtoni kwa Hosea.

Alisema katika mbio hizo wanategemea kuwa na
vyakula vya asili,vinywaji vya asili mbege na kwenye vituo vyao vitakuwa
na vyakula vya kichaga ni wakati mzuri wa kupata uzoefu lengo mbali na
kutangaza utalii na wameshirikisha shule mbalimbali za Msingi na
sekondari .

Balozi huyo alisema wamefanya hivyo wakiamini kwenye
utalii ni vizuri wakihusisha watoto wadogo waweze kujua utalii tokea
wakiwa chini huku akiomba serikali iweze kuangalia suala hilo kwa
kuanzia kufundisha utalii kuanzia shule za Msingi.

“Tumeona
tutangaze utalii kupitia mbio kwani pia ni tiba na kumekuwa na mwamko
mkubwa kwani watanzania hushiriki mbio mbalimbali kupitia hilo
tunawakaribisha watanzania”Alisema ,

“Lakini pia lengo kuanzisha
mbio hizo ni kuunga mkono juhudi ambazo zimeanzishwa na Rais Samia
kwenye kampeni yake ya kutangaza vivutio vya utalii nchini”Alisema

Alisema
Rais amefanya jambo kubwa na nzuri hivyo wao kama wadau wa utalii
wameona watumie fursa ya kuanzisha mbio hizo kwa lengo la kuhakikisha
wanakwenda sambamba na malengo ya Rais Samia.

Awali akingumza
Afisa Uhifadhi kutoka Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro Vitus Mgaya
alisema wameunga na Balozi wa Utalii Lydia ambaye amehamasisha kuandaa
mbio za watu kutembelea ndani ya hifadhi kuendesha baiskeli na shughuli
nyengine za utamadhu wao kama hifadhi wanamuunga mkono kwa juhudi zake
na watamsaoti na watashirikisha watu wengine.

“Mbio hizo ni
nzuri kwa sababu zitakuwa zinatangaza utalii na hivyo kuwafanya
watanzania waweze kufahamu vivutio vyao na kuweza kutangaza utalii waje
waungane Marangu tunawakabisha watanzania wote
wajiandikishe”Alisisitiza.

Naye kwa upande wake Meneja wa Hotel
ya Hosea Inn Marangu Dues Masawe alisema wazo aliloamua kulifanya Balozi
Lydia kwa mbio hizo ni nzuri na watamuunga na kuwataka watanzania
wamsapoti .

Hata hivyo kwa upande wake Fredy Moshi kutoka Ndoro
Water Falls ambao wanaojishughulisha na uhifadhi wa mazingira na
kuotesha miti alisema mbio hizo za zitapita kwenye eneo lao na
wamejiandaa vizuri na wana mshukuru Lidya huku wakiwaomba wadau wengine
wamsapoti wakiwemo Kinapa na Tanapa.

About the author

mzalendoeditor