Featured Kitaifa

CCM YARIDHIA MCHAKATO WA KATIBA MPYA,YAMPONGEZA RAIS SAMIA NA DK.MWINYI

Written by mzalendoeditor

Na Eva Godwin_DODOMA

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Zanzibar Hussein Ali Mwinyi kwa kufanikisha zoezi la uchaguzi katika kulea maridhiano ya kisiasa ambayo yanaendelea, dhamira ikiwa ni kuunganisha Watanzania.

Yamesemwa hayo na Katibu wa Itikadi na Uenezi Ccm Taifa, Shaka Amdu Shaka Leo 22 June, 2022 wakati akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dodoma.

“Rais Samia ni Mwanadiplomasia na ni Mwanasiasa ambae amebobea na nia yake ni kuunganisha Taifa na kuwaleta Watanzania kuwa na Umoja”.amesema Shaka

“Tuendelee kuunga Mkono kwa juhudi za viongozi wetu wa ngazi za juu tunaona maendeleo yanazidi kuwa makubwa katika Chama chetu na Taifa letu”.Amesema Shaka

lakini pia cha Mapinduzi (CCM) kimefanya uteuzi wa Wagombea wa Wenye viti wa Almashauri mbili ikiwa ni Almashauri ya Mji wa Njombe ,Mwenyekiti wa Almashauri ya Ngorongoro sambamba na Mwenyekiti wa Almashauri ya Manispaa ya Moshi.

Yamesemwa hayo na Katibu wa Itikadi na Uenezi Ccm Taifa, Shaka Amdu Shaka Leo 22 June, 2022 wakati akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dodoma.

Amesema Mohamed Festo Bayo ameteuliwa na kamati kuu ya Chama cha amapinduzi (CCM) Kugombea Uwenyekiti Almashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Erasto Mpete ameteuliwa kugombea Uwenyekiti Almashauri ya Mji wa Njombe

“Tangu Tarehe 18 na 19 June tulikuwa na vikao ambavyo vilikuwa vya kisekretarieti vya almashauri kuu Taifa na kufuatia kikao cha kamati kuu kilichofanyika Jana 21 June Mwaka huu na kuhitimisha leo 22 June, 2022” amesema

“Tunayofuraha kubwa kuwajulisha kuwa Chama Cha Mapinduzi Kimefanya uteuzi na kumteua Erasto Mpete kugombea uwenyekiti Almashauri ya Mji wa Njombe pamoja na Mohamed Festo Bayo kugombea Uwenyekiti Almashauri ya Wilaya ya Ngorongoro”.Amesema Shaka.

Lakini Pia CCM imewachagua Zuberi Abdalah Kidumo,Stuati Nathan Mkinda pamoja na Apaikunda Ayo Naburi ,hawa wameteuliwa kugombea nafasi ya Meya Almashauri ya Moshi.

About the author

mzalendoeditor