Featured Kitaifa

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA

Written by mzalendoeditor

Mnamo tarehe 21.06.2022 majira ya saa 06:15 usiku, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya msako huko Njia Panda ya Kasumulu, Kata ya Ibanda, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa BLESSING POFALO MWAGHOGHA [28] Mkazi wa Karonga nchini Malawi akiwa na mali ya wizi Pikipiki aina ya Sanlg, rangi nyekundu ambayo haina namba za usajili yenye Chasis Na. LBLSPJB56N9022623 na Engine Na. SL157FMI22925513 akiwa hana nyaraka zozote zinazomhalalisha kuwa na pikipiki hiyo. Mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani upelelezi wa shauri lake utapokamilika.

KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WA WIZI.

Mnamo tarehe 21.06.2022 majira ya saa 09:30 alasiri, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilipata taarifa toka kwa raia mwema kuwa huko Kijiji na Kata ya Makwale, Tarafa ya Ntebela, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya kumetokea wizi wa “Copawire” katika nguzo za umeme zilizopo Kata ya Makwale.

Kufuatia taarifa hizo, Jeshi la Polisi lilianza kufanya msako mara moja na katika msako huo lilifanikiwa kuwakama watuhumiwa wawili ambao ni:-

  1. LISTO SAMWEL SONY [31] Fundi umeme wa kujitegemea, Mkazi wa Bondeni – Kyela mjini na 
  2. JACOB EDWIN MWANDAMBO [30] Mkazi wa Mbugani – Kyela. 

Katika upekuzi uliofanywa na Jeshi la Polisi kwa watuhumiwa kwa mujibu wa sheria walikutwa wakiwa na vifaa mbalimbali vya kukatia nyaya za umeme ambavyo ni:-

  1. Speaks climb (viatu vya kupandia kwenye nguzo za umeme)
  2. Safety belt (Mkanda wa Usalama wakati wa kupanda kwenye nguzo)
  3. Nyundo 02, 
  4. Bisibisi 02 na 
  5. Priser 01. 

Watuhumiwa na wamehojiwa na kukiri kupanda juu ya nguzo na kukata nyaya za umeme kwa kutumia vitu vyenye makali. Thamani ya uharibifu na hasara iliyosababishwa na watuhumiwa inachunguzwa. Watuhumiwa watafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi wa shauri lao kukamilika.

KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WA KUVUNJA NYUMBA MCHANA NA KUIBA.

Mnamo tarehe 19.06.2022 majira ya saa 07:00 mchana huko Kijiji cha Ilolo, Kata ya Kiwira, Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilipokea taarifa toka kwa HEDSON KAMAGE, Mkazi wa Ilolo – Rungwe kuvunjiwa nyumba yake na kuibiwa TV moja Flat Screen aina ya V-STAR inchi 26.

Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi lilifanya msako na mnamo tarehe 21.06.2022 majira ya saa 06:30 mchana tulifanikiwa kumkamata mtuhumiwa BROWN ASAJILE MWAKYUSA [20] Mkazi wa Simike – Mbeya akiwa na mali ya wizi ambayo ni TV Flat Screen aina ya V-STAR inch 26 yenye thamani ya Tsh. 260,000/= mali ya Mhanga ndugu HEDSON KAMAGE. Mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani upelelezi utapokamilika.

KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WA KUVUNJA DUKA USIKU NA KUIBA.

Mnamo tarehe 20.06.2022 majira ya saa 07:00 usiku, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilipokea taarifa toka kwa JUMA KLALONGO, Mkazi wa Kijiji cha Isumba kuwa alivunjiwa duka lake na kuibiwa TV moja Flat Screen aina ya Mobisol inchi 36 yenye thamani ya Tsh 880,000/=.

Kufuatia tukio hilo, mnamo tarehe 21.06.2022 majira ya saa 06:45 mchana Jeshi la Polisi tulianza msako huko Kijiji cha Isumba, Kata ya Kinyara, Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa BONIPHACE JOSEPH MWANJUGUJU [26] Mkazi wa Isumba akiwa na TV Flat Screen aina ya Mobisol inchi 36 yenye thamani ya Tsh 880,000/= ambayo ni mali ya mhanga JUMA KLALONGO. Mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani mara upelelezi wa shauri lake utapokamilika.

Imetolewa na,

SACP – Ulrich Matei,

Kamanda wa Polisi

MKOA WA MBEYA.

About the author

mzalendoeditor