Featured Michezo

DIRISHA LA USAJILI KWA KLABU ZA LIGI KUU YA NBC CHAMPIONSHIP, FIRST LEAGUE,LIGI KUU YA WANAWAKE YA SERENGETE LITE 2022/23 KUFUNGULIWA JULAI 1,2022

Written by mzalendoeditor
Dirisha la usajili kwa Klabu za Ligi Kuu ya NBC, Championship, First League na Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite msimu wa 2022/2023 litafunguliwa Julai 1, 2022 na kufungwa Agosti 31, 2022.
Katika kipindi hicho Klabu zinatakiwa kukamilisha usajili na uhamisho wa Kimataifa.
Klabu zote zinapaswa kuzingatia muda huo wa usajili, hakutakuwa na muda wa ziada baada ya dirisha kufungwa. Yeyote atakayekutana a changamoto awasiliane na Idara ya Mashindano TFF.
Aidha Dirisha Dogo lenyewe litafunguliwa Desemba 16, 2022 na kufungwa Januari 15, 2023.

About the author

mzalendoeditor