Naibu waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel akiongea wakati alipotembelea hosipitali ya ALMC iliyopo chini ya kanisa la KKKT dayosisi ya Kaskazini kati.
PAMOJA Picha Naibu waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel pamoja na wanafunzi wa chuo Cha uuguzi kilicho chini ya hosipitali ya ALMC
NAIBU waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel akipokea zawadi ya picha aliyopewa na na chuo Cha uuguzi Cha ALMC.
Mkurugenzi wa hosipitali ya ALMC Elisha Twisa akimuonyesha naibu waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel ramani ya namna watakavyoboresha hosipitali hiyo yenye malengo ya kuwa na huduma ya dharura kwaajili ya watalii.
Mwenyekiti wa bodi ya hospitali ya ALMC Dkt John Hillary akiongea wakati naibu waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel alipotembelea hosipitali hiyo.
BAADHI ya watumishi wa Hospitali ya ALMC wakimsikiliza naibu waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel alipotembelea hosipitali
Askofu wa kanisa la KKKT dayosisi ya Kaskazini kati Dkt Solomon Massangwa akiongea wakati naibu waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel alipotembelea hosipitali ya ALMC.
………………………………………………..
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Naibu waziri wa afya Dkt Godwin Mollel huku amezitaka taasisi za dini kujenga vituo vingi vya afya ili kuweza kuisadia serikali katika utoaji wa huduma bora za za afya kwa wananchi pamoja na upatikanaji wa ajira.
Dkt Mollel aliyasema hayo wakati alipotembelea hospitali ya Arusha Lutheran medical center (ALMC) inayomilikiwa na kanisa la kiinjili la kilutheri dayosisi ya Kaskazini kati (KKKT) ambapo alisema kuwa ni vema taasisi za dini kuendelea kujenga vituo vya afya ili kuendelea kuboresha sekta hiyo zaidi pamoja na kuwataka kuendelea kutoa ushirikiano pindi serikali inapowahitaji katika kutimiza malengo waliyojiwekea.
“Taasisi hizi zinapoendelea kutusaidia kuwafikishia huduma za afya kwa wananchi kwetu ni msaada mkubwa kwasababu sekta inaboreshwa lakini pia wananchi wanapata ajira hivyo niwasihi watumishi wa afya kuhakikisha mnatoa huduma bora kwa wagonjwa kwa kutoa lugha nzuri huku mkizingatia weledi pamoja na kufata maadili na sio mfanye mnavyotaka kwasababu mpo sekta binafsi.
“Kwasababu baba Askofu hapa ni mpole na mnyenyekevu mkifanya makosa anashindwa kuwa na maamuzi magumu kama sisi serikali niwahakikishie sisi serikali tutakuwa macho yake huko huko tulipo tutaangalia mtu akifanya jambo linalokiika maadili tutashughulika nae na kumwajibisha,” Alisema Dkt Mollel.
Aidha aliipongeza hospitali hiyo kwanamna walivyopiga hatua katika sula la bajeti ya dawa kutoka milion 70 hadi kufika milioni 119 na ambapo amewataka kuendelea kuongeza ili waweze kukidhi mahitaji ya wagonjwa na ifikapo 2023 bajeti yao ifikie milioni 250.
“Lakini pia nimefirahishwa na utendaji kazi wenu kwani mmeyafanyia kazi yale yote niliyowaachia hivyo endeleeeni kushirikiana na muondoe tofauti zenu na muendelee kufanya kazi kwa umoja ili muweze kufikia malengo mliyoyakusudia,” Alisema Dkt Mollel
Kwa upande wake mkurugenzi wa hospitali hiyo Elisha Twisa alisema kuwa changamoto ya uviko 19 imeathiri maendeleo ya hosipitali hiyo kwa sehemu kubwa kwa kuwa wagonjwa wengine walishindwa kulipa gharama za matibabu kutokana mitungi ya oksijeni kuwa na gahrama za juu.
Alisema kuwa licha ya kutoa huduma bora bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo madeni yaliyosababisha kuchelewa kulipwa kwa mishaahara ya watumishi kodi pamoja na NSSF ambapo Pia ameishukuru serikali kwa kuendelea kuwapatia dawa na kuwaomba kuendelea kutoa ushirikiano ili kuweza kuboresha huduma.
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya hospitali hiyo Dkt John Hillary alisema hospitali hiyo ina malengo makubwa hasa ukizingatia kwa sasa sekta ya utalii imekuwa wanatarajia kujenga hospital kubwa ambayo itaweza kuwahudumia watalii kwa kuwa utalii ukikuwa na sekta ya afya inaboreshwa zaidi
Alifafanua mpango wa hospitali hiyo ni kukua katika utoaji elimu pamoja na huduma bora na kuomba usaidizi kutoka serikalini ili kuhakikisha wanafikia malengo waliyokusudia kwa kuwa hospitali ya kimataifa.