Featured Kitaifa

WATAFITI NELSON MANDELA WAJENGEWA UWEZO WA KUTUNZA BUNIFU ZAO

Written by mzalendoeditor

 Ofisa Mwandamizi Utumishi  na Utawala kutoka Brela Ndg.Raphael Mtalima  wa  Wakala wa  Usajili  wa Biashara na Leseni (BRELA) akielezea kuhusu Umiliki wa Uvumbuzi (Intellectual Property) katika  warsha ya kuwajengea uwezo Watumishi na watafiti kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Juni 13 ,2022 Jijini Arusha.

Menaja Usimimazi wa Bunifu katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Ndg. Joseph Swai akielezea jambo katika warsha ya kuwajengea uwezo Watumishi na Watafiti wa Taasisi hiyo  iliyoandaliwa kwa kushirikiana na Wakala wa  Usajili  wa Biashara na Leseni (BRELA) Juni 13 ,2022 Jijini Arusha.

Ofisa Mwandamizi Utumishi na Utawala wa  Wakala wa  Usajili  wa Biashara na Leseni (BRELA) Ndg.Raphael Mtalima (kushoto) akimsikiliza Menaja Usimimazi wa Bunifu katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Ndg. Joseph Swai (kulia) wakati wa  warsha ya kuwajengea uwezo Watumishi na Watafiti kutoka Taasisi hiyo Juni 13 ,2022 Jijini Arusha.

…………………………………………………………

Watumishi na watafiti kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela wajengewa uwezo wa  namna ya kutunza tafiti na bunifu zao kupitia warsha ya siku moja iliyoandaliwa kwa ushirikiano  na  Wakala wa  Usajili  wa Biashara na Leseni (BRELA)  Juni 13 ,2022 Jijini Arusha.

Akizungumza katika warsha hiyo  Ofisa Mwandamizi Utumishi  na Utawala kutoka Brela Ndg. Raphael Mtalima alisema kuwa  wabunifu  na wavumbuzi  wanavumbua bunifu zao  lakini hawajui wazilinde vipi  na hivyo kutokufaidika na matunda ya vumbuzi hizo.

 Anazidi kueleza kuwa,  katika kuhakikisha wabunifu na watafiti wanapata uelewa  kuhusu Umiliki wa Uvumbuzi (Intellectual Property ) Brela imeamua kutoa elimu  katika vyuo vitano vilivyopo  jijini Arusha ikiwemo Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia  ya Nelson Mandela iliyojikita katika masuala  ya kisayansi.

“Tunawajengea uwezo wabunifu wajue umuhimu wa kuendelea na tafiti zao na kuzisajili BRELA kwa ajili ya kunufaika nazo hapo baadaye”amesema Ndg. Raphael.

Naye Mkuu wa Idara ya Utafiti na Ubunifu  katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela , Dr. Edna Makule alisema warsha hiyo ina  manufaa makubwa kwa watafiti na wabunifu  kutoka katika taasisi hiyo kwa kuwa tayari imefanya  tafiti na bunifu mbalimbali zilizofikia hatua  ya kulindwa,  kupitia elimu waliyoipata itasaidia  kupiga hatua zaidi katika kulinda bunifu hizo.

Kwa upande wake Mwanafunzi anayechukua  masomo ya Shahada ya Uzamivu (PhD), Isack Kandola alisema amejifunza  mambo mengi  kupitia warsha hiyo  na kuahidi kufanyia kazi na kutoa elimu kwa wengine waliokosa fursa ya kuhudhuria ili kulinda bunifu zao zisiibiwe.

Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela ni Taasisi inayotoa elimu kwa ngazi ya Shahada ya Uzamili( Masters) na Uzamivu (PhD) katika masuala ya sayansi  na teknlojia. 

About the author

mzalendoeditor