Featured Kitaifa

TAASISI YA MAFUNZO YA UANASHERIA KWA VITENDO TANZANIA  KUANZISHA KOZI MPYA YA WASAIDIZI WA SHERIA

Written by mzalendoeditor

Na Eva Godwin-DODOMA

WAKAZI wa Dodoma na Mikoa ya jirani wameomba kufika katika uwanja wa Jamhuri kujifnuza na kujionea kazi nzuri zinazofanywa na Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School of Tanzania).

Hayo yameelezwa na Mkufunzi wa Taasisi hiyo Paul Rambau wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika uwanja wa jamhuri ambapo maonesho ya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi Stadi yanaendelea.

Amewaomba wananchi waje kwenye banda la Law school of Tanzania kuja kufunza mambo mbalimbali kuhusiana na sheria pamoja na kazi nzuri zinazofanywa katika taasisi hiyo.

“Law school of Tanzania mwaka huu tumedhamiria kuanzisha Kozi mpya kwa ajili ya wasaidizi wa sheria na dirisha lipo wazi kwa sasa tupo kwa ajili yenu “,amesema Rambau

“Tumeamua kuongeza wigo wa mafunzo yetu kwa kutengeneza mafunzo maalumu kwa wasaidizi wa kisheria kwa kuona idadi kubwa ya watanzania wanahuitaji huo”

Rambau amesema taasisi hii ina uzoefu na walimu wa kutosha waliobobea katika uzoefu wa kuendesha mafunzo kwa vitendo na imezalisha mawakili bora Nchini Tanzania.

“Tuna uzoefu wa kutosha kwa kufanya mafunzo kwa vitendo na pia mawakili bora wamezalishwa kutoka katika chuo chetu,na ukitoka chuo chetu ajira ni nje nje.

“Na mafunzo hayo yatatolewa kwa Mwaka Mmmoja ambapo mwanafunzi atakaa darasani kwa miezi mitano na miezi mitano mingine mwanafunzi ataenda kwenye taasisi nyingine za kiserikali kwaajili ya vitendo”,amesema .

About the author

mzalendoeditor