Featured Michezo

TIMU ZA SERENGETI GIRLS NA TEMBO WARRIORS WAPEWA HESHIMA YA MASHUJAA TAIFA NA BUNGE

Written by mzalendoeditor

 
SPIKA
wa Bunge Tulia Ackson akizungumza Bungeni wakati wa Timu ya wanawake ya
soka chini ya umri wa miaka 17 (Serengeti Girls) ilipowasili bungeni

Na John Mapepele  
Timu
ya wanawake ya soka chini ya umri wa miaka 17 (Serengeti Girls)
imeweka  historia  ya kuwa  timu ya  kwanza kupewa heshima na Bunge la
Jamhuri ya Muungano kuingia  na kukaa kwenye viti vya mawaziri ndani ya
bunge  baada ya kufuzu kuingia  mashindano ya dunia ikiwa ni heshima ya
mashujaa wa Taifa kwa kazi kubwa iliyoifanya ambapo kesho ni zamu ya
Timu ya soka ya Taifa ya Walemavu ya (Tembo Warriors) ambayo pia
imefuzu  mashindano ya dunia ya soka kwa walemavu.
Akiongea 
 mara baada ya kuketi eneo hilo rasmi la mawaziri, Waziri mwenye
dhamana ya Michezo nchini. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema ushindi huo
unatokana  na jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kuiwezesha  timu
hiyo katika kipindi chote cha  maandalizi wa  mashindano hayo.
“Namshukuru
Rais wa Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan kwa
kutuwezesha, kututia moyo na kutufuatilia kwa karibu sana katika kipindi
chote” amefafanua Mhe. Mchengerwa.
Aidha,
amesema Serikali itahakikisha inaendelea kuisaidia timu hiyo ili iweze
kwenda  na kushinda kwenye mashindano hayo hatimaye kurejesha kombe
hilo  la dunia na kuwataka wadau mbalimbali kushirikiana na Serikali
katika kuwatia moyo  na kuwasaidia ili washinde.
Akizungumzia
jinsi  timu ilivyopambana hadi kufika hapo amesema  kuwa  timu ilianza
kuchabanga  Botswana magoli 11-0, ikaitandika  Burundi jumla ya magoli
6-1, na ikamalizia na kuibamiza timu ya Cameroon jumla ya magoli 5-1.
Kwa
upande wa Warriors amesema iliishindilia Cameroon mabao 5-0, kabla ya
kuikandamiza Senegal goli 1-0 na kuichakaza Morroco magoli 2-0.
Ameongeza
kuwa dhamira ya Serikali ni kuendelea kufanya mapinduzi makubwa katika
sekta za michezo na Sanaa ili kuipeleka Tanzania kimataifa ambapo
amefafanua kuwa kuanzia Februari mwaka huu timu zote za taifa
zinazoshiriki kwenya mashindano ya kimataifa  zimewekwa kambini na
zinagharimiwa na Serikali.
Kwa
upande wake Nahodha wa timu hiyo Noela Luhala alipewa heshima ya
kuzungumza mbele ya Bunge tukufu ambapo amesisitiza kuwa kama ilivyo kwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano. Mhe, Mama Samia Suluhu Hassan kuwa
mwanamke wa kwanza kuwa Rais nchini ni ndoto za muda mrefu kwa timu hiyo
kuwa ya kwanza kuingia mashindano ya Kombe la Dunia na kuwa Timu ya
kwanza kulileta kombe hilo nchini.
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania. Mhe Tulia Ackson ameipongeza timu hiyo
kwa  niaba  ya bunge zima na kuwataka  kurejea na kombe hiyo  kwenye
mashindano hayo.

About the author

mzalendoeditor