Featured Kitaifa

UTEUZI:RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:

  1. Amemteua Dkt. Leonada Raphael Mwagike kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Ununuzi wa Umma (PPRA).  Dkt. Mwagike ni Mtaalam wa Ununuzi na Ugavi, Chuo Kikuu cha Mzumbe, Morogoro. Uteuzi wa Dkt. Mwagike utaanza tarehe 21 Julai, 2022 baada ya Mwenyekiti aliyepo Balozi Dkt. Martern Lumbanga kumaliza kipindi chake cha pili tarehe 20 Julai, 2022.

2.Amemteua Luteni Jenerali (Mstaafu) Samwel Albert Ndomba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Mzinga. Luteni Jenerali (Mstaafu) Ndomba ameteuliwa kwa kipindi cha pili cha miaka mitatu kuanzia tarehe 02 Juni, 2022.

3.Amemteua Jaji Mustafa Kambona Ismail kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Masoko ya Mitaji na Dhamana Tanzania. Jaji Ismail anachukua nafasi ya Jaji Fredinand Wambali ambaye aliteuliwa kuwa Jaji wa Rufani. Uteuzi huu umeanza tarehe 02 Juni, 2022. 

About the author

mzalendoeditor