Featured Kitaifa

MAJALIWA ATOA MAAGIZO 15 YA UHIFADHI WA MAZINGIRA NCHINI

Written by mzalendoeditor

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wadau mbalimbali walioshiriki kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa yamefanyika leo Juni 5,2022 jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt Selemani Jafo,akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa yamefanyika leo Juni 5,2022 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga,akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa yamefanyika leo Juni 5,2022 jijini Dodoma.

Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini,Bw. Zlatan Milišić,akielezea hali ya mazingira Duniani wakati wa  kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa yamefanyika leo Juni 5,2022 jijini Dodoma.

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akitoa salamu za Mkoa wake wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa yamefanyika leo Juni 5,2022 jijini Dodoma.

VIONGOZI,Mabalozi wa Mazingira,Wadau pamoja na Wanafunzi wakifatilia hotuba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (hayupo pichani) akizungumza  wakati wa  kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa yamefanyika leo Juni 5,2022 jijini Dodoma.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua  Mpango Kabambe wa Uhifadhi wa Mazingira, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani,kitaifa yamefanyika leo Juni 5, 2022 jijini Dodoma. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Selemani Jafo na kulia ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini,Bw. Zlatan Milišić.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionesha Mpango Kabambe wa Uhifadhi wa Mazingira baada ya kuuzindua, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, yamefanyika leo Juni 5,2022 jijini Dodoma. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Selemani Jafo na kulia ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini,Bw. Zlatan Milišić,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Selemani Jafo akipokea kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan Tuzo ya Mazingira kwa viongozi wakuu wa Serikali kutoka kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, yaliyofanyika Kitaifa leo Juni 5,2022 Jijini Dodoma. kulia ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini,Bw. Zlatan Milišić.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akipokea Tuzo ya Mazingira  kutoka kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, yaliyofanyika Kitaifa leo Juni 5,2022 Jijini Dodoma. 

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Queen Sendiga, akipokea Tuzo ya Mazingira kutoka kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, yaliyofanyika Kitaifa leo Juni 5,2022 Jijini Dodoma. 

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt Selemani Jafo,akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Ofisi ya Makamu wa Rais na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) mara baada ya  kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa yamefanyika leo Juni 5,2022 jijini Dodoma.

……………………………………..

Na Alex Sonna-DODOMA

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa  ametoa maagizo 15 kwa wizara, taasisi na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhusu uhifadhi wa mazingira nchini na kutaka yatekelezwe kikamilifu.

Waziri Mkuu aametoa maagizo hayo leo Juni 5,2022 jijini Dodoma  wakati akizungumza na wadau mbalimbali walioshiriki kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa yamefanyika jijini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema Mpango Kabambe wa Mazingira utengewe bajeti ya kila mwaka kwa kipindi chote cha utekelezaji wake wa miaka 10.

‘Wizara ya Fedha na Mipango inapaswa ihakikishe  Mpango Kabambe wa Usimamizi na Hifadhi ya Mazingira unakuwa sehemu ya vipaumbele vya bajeti vya kila mwaka kwa kipindi chote cha utekelezaji wake wa miaka 10.’amesema Waziri Mkuu

Amesema Wizara za kisekta, Mamlaka za Serikali za Mitaa zinapaswa zihakikishe Mpango Kabambe wa Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira unajumuhishwa katika mipango na Bajeti zao, sambamba na kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara na kuwasilisha taarifa ya utekelezaji Ofisi ya Makamu wa Rais.

 “Kila Mamlaka ya Serikali za Mitaa ihakikishe maeneo yote yaliyoharibiwa yanarejeshwa kwa kupandwa miti upya na kila Mamlaka ya Serikali za Mitaa ihakikishe inatekeleza vema programu ya kitaifa ya upandaji miti 1,500,000 ili kuhakikisha nchi yetu inakuwa ya kijani,” amesisitiza.

Amezitaka wizara, taasisi, mashirika ya Serikali na binafsi yanayotumia nishati ya kuni na mkaa kwa ajili ya kupikia au shughuli nyingine za uzalishaji zianze kutumia nishati mbadala na kwamba kila Mamlaka ya Serikali za Mitaa ihakikishe inadhibiti matukio ya uchomaji ovyo misitu.

Waziri Mkuu amezitaka taasisi za utafiti na vyuo vya elimu ya juu ziendelee kufanya tafiti za nishati mbadala ili kuondokana na utegemezi wa nishati ya kuni na mkaa kwa kupikia. Vilevile, ametaka zifanyike tafiti za namna ya kuzuia na kudhibiti kuenea kwa viumbe vamizi vinavyochangia uharibifu wa mazingira nchini.

Kuhusu takataka, amezitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa ziweke utaratibu wa kuhakikisha taka zinatenganishwa na zinakusanywa na zile zinazohusika na usimamizi wa mifereji ya maji ya mvua mijini kuhakikisha mifereji hiyo inasafishwa ili kupunguza matukio ya mafuriko.

Waziri Mkuu amesema kila Mamlaka ya Serikali za Mitaa ihakikishe maeneo yaliyotengwa kwa matumizi ya misitu ya mijini katika mamlaka zao hayabadilishwi matumizi wala kuvamiwa.

“Sekta zinazohusika zihakikishe kuwa ardhi na uoto asili katika vyanzo vya maji, vilima na milima iliyo katika maeneo yao inalindwa na kuhifadhiwa ili kuzuia mmomonyoko wa udongo na kukauka kwa vyanzo hivyo vya maji,” ameongeza na kusisitiza kuwa vilima vinavyozunguka mji wa Dodoma vihifadhiwe.

Waziri Mkuu amezitaka sekta zinazohusika na usimamizi wa shughuli za umwagiliaji mashamba zihakikishe kunakuwepo matumizi sahihi ya maji yenye kuzingatia uhifadhi na ulinzi wa mazingira.

Waziri Mkuu amezitaka mamlaka zinazohusika na usimamizi wa hifadhi za wanyamapori zidhibiti matukio ya ajali za barabarani kwa wanyamapori, na pia zidhibiti shughuli za binadamu pamoja na uvamizi katika maeneo ya mapito ya wanyamapori (shoroba) ili kupunguza uharibifu wa mazao, mali na binadamu kupoteza maisha kutokana na kuwepo mwingiliano wa wanyama na binadamu.

Hata hivyo Waziri Mkuu amekemea tabia ya uchomaji miti, uvamizi na uharibifu wa mapori tengefu, ukataji wa miti holela kwa ajili ya uchomaji wa mkaa, uvamizi na uharibifu wa vyanzo vya maji pamoja na uchomaji moto misitu.

“Kutokana na kuongezeka kwa uharibifu wa mazingira, ninaagiza Wizara na taasisi husika, pamoja na wananchi kwa ujumla, kuimarisha ushirikiano katika kukomesha uvamizi na uharibifu wa mapori tengefu kote nchini. Ninawasihi wananchi tutoe ushirikiano wa kutosha kuhakikisha tunarejesha misitu, ikolojia na uoto wa asili katika maeneo yetu, hususan maeneo ambayo miti ya asili iko kwenye tishio la kutoweka. Tuwe walinzi wazuri wa mazingira kwa faida ya kizazi hiki na kijacho,” amesisitiza.

“Nimejulishwa kuwa maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani mwaka huu yanaendana na uzinduzi wa Mpango Kabambe wa Hifadhi ya Mazingira ni matarajio yangu Mpango huo utakuwa ni nyenzo muhimu ya uibuaji, utekelezaji na usimamizi wa miradi ya mazingira nchini,”amesema.

Waziri Mkuu amezindua Mpango Kabambe wa Hifadhi ya Mazingira na kutoa tuzo kwa Mabalozi wa Mazingira na viongozi wakuu watano akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

Kwa Upande wake Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt Selemani Jafo amesema kuwa katika Maadhimisho ya siku ya Mazingira itatoa hali ya kutafakari kwa kina umuhimu wa kutunza Mazingira katika nchi wanachama kwa Kutoa elimu juu ya uhifadhi na kutunza Mazingira kwa ujumla.

Dkt. Jafo amesema ofisi yake imezindua mpango wa soma na mti ambapo kila mwanafunzi anapaswa kupanda mti mmoja.

“Tumezindua kampeni ya Soma na Mti ambapo wanafunzi milioni 14.5 kutoka shule za msingi, sekondari na vyuo vikuu wameshiriki kwa kupanda mti mmoja mmoja.

“Maadhimisho ya mwaka huu yatafanyika nchini Sweden ambapo nchi hiyo ilikuwa ni mwenyeji wa mkutano wa kwanza wa umoja wa mataifa kwa kongamano la kwanza la masuala ya Mazingira,

Kaulimbiu ya mwaka huu inasema DUNIANI NI MOJA kauli hiyo inatabananisha kuwa dunia ni yetu sote na hakuna mbadala wake hivyo hatuna budi kuyatunza na kuhifadhi Mazingira yake ili iendelee kutuletea mahitaji ,” amesema Waziri Jafo.

About the author

mzalendoeditor