Featured Kitaifa

FEDHA ZA MIRADI ZIENDANE NA THAMANI YA MRADI- MWAKITALIMA

Written by mzalendoeditor
Timu ya ufatiliaji wa zoezi la usimamizi wa mradi wa Huduma Endelevu za Maji na Usafi wa Mazingira vijijini, kutoka Wizara ya Afya ikiongozwa na Anyitike Mwakitalima ikiwa katika kata ya Zahanati ya Ndung’unyi iliyopo halmashauri ya wilaya ya Ikungi Mkoani Singida ikikagua vyoo vilivyojengwa kwa kutekeleza mradi.
Timu ya ufatiliaji wa zoezi la usimamizi wa mradi wa Huduma Endelevu za Maji na Usafi wa Mazingira vijijini, kutoka Wizara ya Afya ikiongozwa na Anyitike Mwakitalima ikiwa katika kata ya Nkuhi iliyopo halmashauri ya wilaya ya Ikungi Mkoani Singida kufatilia utekelezaji wa mradi.
Muonekano wa sehemu ya kunawia mikono iliyojengwa chini ya utekelezaji wa mradi wa Huduma Endelevu za Maji na Usafi wa Mazingira vijijini katika zahanati ya Ndung’unyi hamashauri ya wilaya ya Ikungi mkoani Singida
Muonekano wa Tanki la kuifadhi maji safi na salama vilivyo tekelezwa chini ya mradi wa Huduma Endelevu za Maji na Usafi wa Mazingira vijijini katika Zahanati ya Ndung’unyi wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida
Timu ya ufatiliaji wa zoezi la usimamizi wa mradi wa Huduma Endelevu za Maji na Usafi wa Mazingira vijijini, kutoka Wizara ya Afya ikiongozwa na Anyitike Mwakitalima ikiwa katika kata ya Zahanati ya Ndung’unyi iliyopo halmashauri ya wilaya ya Ikungi Mkoani Singida ikikagua vyoo vilivyojengwa kwa kutekeleza mradi.Timu ya ufatiliaji wa zoezi la usimamizi wa mradi wa Huduma Endelevu za Maji na Usafi wa Mazingira vijijini, kutoka Wizara ya Afya ikiongozwa na Anyitike Mwakitalima ikiwa katika kata ya Zahanati ya Ndung’unyi iliyopo halmashauri ya wilaya ya Ikungi Mkoani Singida ikikagua vyoo vilivyojengwa kwa kutekeleza mradi
…………………………………….
Na. WAF, IKUNGI – SINGIDA
Mratibu wa Mradi wa Huduma Endelevu wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini, kutoka Wizara ya Afya Ndg. Anyitike Mwakitalima ameitaka mikoa 17 na Halmashauri 86 nchini zinazotekeleza mradi wa Huduma Endelevu za Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (Sustainable Rural Water Supply and Sanitation) kuhakikisha kazi zinazotekelezwa chini ya mradi huo zinakua na thamani inayo akisi fedha iliyotolewa yaani “Value for Money”.
Mwakitalima ametoa kauli hiyo leo wakati akiendelea na zoezi la usimamizi wa mradi wa Huduma Endelevu za Maji na Usafi wa Mazingira vijijini, katika halmashauri ya wilaya ya Ikungi Mkoani Singida ambapo amesema fedha iliyotolewa iwe na uwiano sawa na kazi iliyofanyika ili kuongeza tija ya mradi huo kwa wananchi wa eneo husika.
“Nasisitiza kwa ujumla Halmashauri zote zinazotekeleza mradi huu kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi kwani inaonekana wako nyuma na sisi tunataka mradi ukamilike kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa wananchi”. Amesisitiza Mwakitalima.
Vile vile Mwakitalima ameongeza kuwa halmashauri hizo zinatakiwa kuhakikisha kunafanyika usimamizi wa karibu ili kuleta ufanisi katika utekelezaji wa mradi.
Pia Mwakitalima amekumbushia baadhi ya shughuli zilizokuwa zimesaulika nazo ziweze kufanyiwa kazi ili kuleta ukamilifu wa mradi na kwa manufaa makubwa yaliyokusudiwa.
Aidha, Mwakitalima amemtaka Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Puma iliyopo katika kata ya Puma Halmashauri ya Ikungi kuhakikisha ifikapo Jumanne ya wiki ijayo vyoo vilivyojengwa chini ya mradi wa Huduma Endelevu za Maji na Usafi wa Mazingira vijijini mwaka jana vinaanza kutumiwa na wananchi wanaofata huduma katika zahati hiyo.
“Haiwezekani vyoo vimekamilika tangu mwaka jana na mfumo wa maji upo vizuri halafu havitumiki eti mnasubiri vizinduliwe, hakuna kitu kama hicho vyoo vitoe huduma kwa wananchi ili kuleta manufaa yaliolengwa katika mradi”. Ameeleza Mwakitalima.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Ndung’unyi, iliyopo katika kata ya Ndung’unyi Halmashauri ya Ikungi, Mkoa wa Singida, Dkt. Advera Thadeo amesema anaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia fedha kiasi cha shilingi Milioni 20 kupitia mradi wa Huduma Endelevu za Maji na Usafi wa Mazingira vijijini kwa ajili ya kutekeleza ujenzi wa vyoo vitatu ikiwemo choo cha walemavu, kuweka mfumo wa maji safi katika sehemu zote za kutolea huduma pamoja na sehemu za kunawia mikono.
“Mpaka sasa utekelezaji wa mradi huu umefikia asilimia 97 na mafundi wanaendelea na kazi kukamilisha asilimia tatu zilizobaki ili mradi ukamilike kwa wakati na kuanza kutoa huduma kama yalivyo matarajio ya mradi wenyewe”, ameeleza Dkt. Advera
Dkt. Advera ameongeza kuwa mradi huo ukikamilika utakuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi wa kata ya Ndung’unyi pamoja na watumishi wa zahanati hiyo kwani changamoto itakua imetatuliwa na kuleta ufanisi wa utoaji huduma kwa wananchi.

About the author

mzalendoeditor