Meneja wa Mfumo wa Usimamizi wa Rasirimali za Barabara TANROADS, Mhandisi Mussa George akikagua Mashine ya kuhesabu idadi ya magari barabarani (Inductive Loop Vehicle Counters) mara baada ya kukifunga katika barabara ya Morocco-Mwenge Jijini Dar es salaam.
Meneja wa Mfumo wa Usimamizi wa Rasirimali za Barabara TANROADS, Mhandisi Mussa George akizungumza na waandishi wa habari katika barabara ya Morocco-Mwenge Jijini Dar es Salaam mara baada ya kukagua mashine ya kuhesabu idadi ya magari barabarani (Inductive Loop Vehicle Counters) ambayo wameifunga hivi karibuni. Mashine ya kuhesabu idadi ya magari barabarani (Inductive Loop Vehicle Counters) ikiwa imefungwa katika barabara ya Morocco-Mwenge Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
*********
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
SERIKALI kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS)wamefanikiwa kufunga Mashine ya kuhesabu idadi ya magari barabarani (Inductive Loop Vehicle Counters) katika barabara ambazo magari yyanapita kwa wingi ili kusaidia katika usanifu na ujenzi wa barabara.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 02,2022 Jijini Dar es Salaam, Meneja wa Mfumo wa Usimamizi wa Rasirimali za Barabara TANROADS, Mhandisi Mussa George amesema kwa kawaida TANROADS inakuwa na utaratibu wa kuhesabu magari kwa kutumia watu hivyo kupitia kifaa hicho kitawarahishishia ufanyaji kazi na kuepuka muda na gharama kubwa.
Amesema kupitia teknolojia hiyo inasaidia kupata data ambazo zinauharisia kuliko mwanzo walivyokuwa wanatumia watu ambapo mara nyingi hutumia kwa muda tu wakati mashine hiyo itatumika kwa masaa 24 na kuleta data zilizo sahihi.
“Lengo la kuhesabu magari , Huwa tunatumia taarifa za magari kwenye kufanya usanifu wa barabara na kufanya mateengenezo pia .Siku zote unapofanya usanifu wa barabara lazima ujue idadi ya magari yanayopita kwenye hiyo sehemu na baada ya kupata idadi ya magari na aina ya magari ndo inakusaidia kwenye tabaka la barabara kwamba barabara unayoijenga iwe ya aina gani”. Amesema Bw.George.
Aidha amewataka watanzania hasa madereva kuhakikisha wanalinda miundombinu inayotekelezwa na serikali na itakapotokea mtu au watu wakifanya uharibifu kwenye miundombinu hii basi watachukuliwa hatua.
“Kanda ya Ziwa tulipata kesi tatu za uharibifu na wizi wa hizi mashine na kwa hapa DDar es Salaam tulipata kesi moja na kwa bahati nzuri maaskari walikuwa karibu walijaribu kusaidia ,tunawaomba wanancchi tuzilinde hizi mashine”. Amesema
Pamoja na hayo amesema wamenunua mashine hizo 150 kwa nchi nzima na inashauriwa mashine hizo zifungwe kwenye barabara za lami ambapo kwasasa wamefunga mashine 50 kwaajili ya kuanzia ambazo wamezifunga nchi nzima na kipaumbele cha kwanza wameipa barabara kuu pili barabara za mijini ikiwemo mkoa wa Dar es Salaam ambapo wamefunga mashine 16.