Featured Kitaifa

WAZIRI MKUU:’WATANZANIA TUILINDE NA KUTUNZA MISITU YETU’

Written by mzalendoeditor

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika Mji wa Serikali, eneo la Mtumba kwa ajili ya zoezi la upandaji wa miti  hafla iliyofanyika leo Juni 1,2022 jijini Dodoma.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,akiwapugia mkono wananchi (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili katika Mji wa Serikali, eneo la Mtumba kwa ajili ya zoezi la upandaji wa miti  hafla iliyofanyika leo Juni 1,2022 jijini Dodoma.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,akizungumza wakati alipozindua zoezi la upandaji wa miti katika Mji wa Serikali, eneo la Mtumba jijini Dodoma hafla iliyofanyika leo Juni 1,2022.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akizungumza wakati wa  zoezi la upandaji wa miti katika Mji wa Serikali, eneo la Mtumba jijini Dodoma hafla iliyofanyika leo Juni 1,2022.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja,akizungumza wakati wa  zoezi la upandaji wa miti katika Mji wa Serikali, eneo la Mtumba jijini Dodoma hafla iliyofanyika leo Juni 1,2022.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu wenye ulemavu. Ummy Ngeliananga ,akizungumza wakati wa  zoezi la upandaji wa miti katika Mji wa Serikali, eneo la Mtumba jijini Dodoma hafla iliyofanyika leo Juni 1,2022.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Dkt. John Jingu,akizungumza wakati wa  zoezi la upandaji wa miti katika Mji wa Serikali, eneo la Mtumba jijini Dodoma hafla iliyofanyika leo Juni 1,2022.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akizungumza wakati wa  zoezi la upandaji wa miti katika Mji wa Serikali, eneo la Mtumba jijini Dodoma hafla iliyofanyika leo Juni 1,2022.

SEHEMU ya Viongozi,Mabalozi wa Mazingira pamoja na wananchi wakifatilia hotuba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (hayupo pichani) wakati wa  zoezi la upandaji wa miti katika Mji wa Serikali, eneo la Mtumba jijini Dodoma hafla iliyofanyika leo Juni 1,2022.

Wasanii wa kikundi cha Mchoya kutoka Chalinze Nyama Dodoma wakicheza ngoma ya asili ya kabila la Wagogo katika hafla ya uzinduzi wa zoezi la upandaji miti katika Mji wa Serikali, eneo la Mtumba jijini Dodoma Juni 1, 2022. Mgeni rasmi alikuwa ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa .

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua zoezi la upandaji wa miti katika Mji wa Serikali, eneo la Mtumba jijini Dodoma, Juni 1, 2022. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Selemani Jafo na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akipanda miti katika Mji wa Serikali, eneo la Mtumba jijini Dodoma, leo Juni 1, 2022.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akipanda miti katika Mji wa Serikali, eneo la Mtumba jijini Dodoma, Juni 1, 2022.

……………………………………….

Na Alex Sonna-DODOMA

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa,amesema Serikali ya Awamu ya Sita imeweka kipaumbele katika utunzaji wa misitu kwa kutekeleza azma ya uhifadhi na uendelezaji misitu kwa vitendo.

Waziri Mkuu ameyasema hayo  leo Juni 1,2022 wakati akizindua  zoezi la upandaji wa miti katika Mji wa Serikali, eneo la Mtumba jijini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema kuwa Jitihada  za Serikali ni kuweka msisitizo wa uhifadhi wa mazingira ili kutkeleza  mikakati mbalimbali pamoja na maboresho ya Sera na Sheria ili ziwiane na mahitaji ya sasa ya kitaifa, kikanda na kimataifa. 

“Nchini zipo kampeni na mikakati mbalimbali inayolenga kutekeleza suala la uhifadhi wa mazingira ikiwemo Kampeni ya Upandaji Miti milioni 1.5 kwa Kila Halmashauri kwa Mwaka,”amesema  Majaliwa. 

Aidha amesema kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais na Ofisi ya Rais, TAMISEMI imeendelea kuratibu utekelezaji wa kampeni ya kitaifa ya upandaji na utunzaji wa miti inayotekelezwa nchini kwa kila Halmashauri kupanda miti milioni 1.5 kila mwaka.

“Katika kipindi cha mwaka 2020/21, idadi ya miti iliyopandwa ni 202,923,907 na iliyostawi ni 165,501,119 sawa na asilimia 81.6. Halmashauri 27 kati ya 184 zilivuka lengo la kupanda miti milioni 1.5 kwa mwaka,”alisema Waziri Mkuu.

Hata hivyo amesema  kuwa Katika kipindi cha mwaka 2021/22, Serikali imeendelea kuratibu utekelezaji wa Kampeni ya Kukijanisha Dodoma. 

“Katika kipindi hicho Jumla ya miti 692,247 ilipandwa katika wilaya zote za Mkoa wa Dodoma kama ifuatavyo: Dodoma Mjini miti 584,790; Wilaya ya Mpwapwa miti 21,450; Wilaya ya Bahi miti 20,720; Wilaya ya Chemba miti 4,000; Wilaya ya Kongwa miti 45,587; Wilaya ya Kondoa miti 11,200; na Wilaya ya Chamwino miti 4,500,

Waziri Mkuu amesema kuwa Amwaka huu mpango huo utazinduliwa tarehe 05 Juni, 2022 siku ya Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira, Duniani.

Pia ameeleza kuwa Serikali imeendelea kuhamasisha upandaji miti kupitia Kampeni ya Soma na Mti iliyozinduliwa tarehe 20 Januari, 2022 katika Jiji la Dodoma. 

“Kampeni hiyo imelenga kujenga tabia kwa wanafunzi wa Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo nchini kushiriki kikamilifu katika upandaji na utunzaji wa miti,Kampeni imeendelea kuhamasishwa na Wakuu wa Mikoa na Wilaya; na Mabalozi wa Mazingira katika mikoa mbalimbali nchini,Jitihada hizi zote zinafanywa kwa kutambua umuhimu wa kupanda miti ili kuimarisha uhifadhi wa mazingira kwa maendeleo endelevu nchini,”ameeleza Waziri Mkuu.

Kwa Upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo,amesema kuwa katika Maadhimisho ya siku ya Mazingira itatoa hali ya kutafakari kwa kina umuhimu wa kutunza Mazingira katika nchi wanachama kwa Kutoa elimu juu ya uhifadhi  na kutunza Mazingira kwa ujumla.

“Maadhimisho ya mwaka huu yatafanyika nchini Sweeden ambapo nchi hiyo ilikuwa ni mwenyeji wa mkutano wa kwanza wa umoja wa mataifa kwa kongamano la kwanza la masuala ya Mazingira’

Kaulimbiu ya mwaka huu inasema DUNIANI NI MOJA kauli hiyo inatabananisha kuwa dunia ni yetu sote na hakuna mbadala wake hivyo hatuna budi kuyatunza na kuhifadhi Mazingira yake ili iendelee kutuletea mahitaji ,”amesema Waziri Jafo.

Awali  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu wenye ulemavu. Ummy Ngeliananga ,amesema kuwa kama nchi katika zoezi la upandaji wanaungana na wenzao duniani kuhakikisha tunaendelea kulinda. Mazingira yetu Kama taifa

“Tunafahamu kwamba Suala la Mazingira ni ageda ya kidunia  kwani hata Rais wa awamu ya Sita Samia Suluhu Hassan na Makamu wake Dkt Philip Mpango wameweza kuudhuria mikutano mikubwa mbalimbali ya Kimataifa nawameonekana wakizungumzia agenda hiyo ya upandaji miti kwa mapana,” amesema.

About the author

mzalendoeditor