Featured Kitaifa

WAZIRI GWAJIMA ATAKA WANAWAKE KUWA VINARA KUKEMEA UKATILI

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Mhe. Dorothy Gwajima akizungumza na Wanawake vinara walipotembelea Ofisi za Wizara jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akizungumza wakati kikao cha Wizara na Wanawake vinara walipotembelea Ofisi za Wizara jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt Zainab Chaula akielezea jambo wakati wa kikao cha Wizara na Wanawake vinara walipotembelea Ofisi za Wizara jijini Dodoma.

Mmoja wa wanawake vinara Dkt. Herieth Mkangaa akieleza changamoto zinazowakabili Wanawake hasa wajasirimali wakati wa kikao kati yao na Viongozi wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum 

jijini Dodoma.

Baadhi ya Wanawake vinara wakifuatilia mambo mbalimbali wakati wa kikao kati yao na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum jijini Dodoma.

Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WMJJWM

……………………………………………………..

Na WMJJWM-Dodoma

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Mhe. Dorothy Gwajima amewataka Wanawake kuwa vinara kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto nchini.

Dkt. Gwajima ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na Wanawake vinara walipotembelea katika Ofisi za Wizara.

Dkt. Gwajima alisema elimu zaidi kwa kutumia wataalam wa Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii itumike kubadilishabfikra za jamii ili iweze kushiriki kataka kupambana na vitendo vya ukatili hasa kwa jamii kujikita kunako mapambano hayo hasa kuchangia rasilimali fedha na nguvu kazi ili kuondokana na vitendo hivyo. 

Ameongeza kuwa Wanawake wanatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuwalinda Watoto na vitendo vya ukatili hasa unaotokea nyumbani na shuleni kwa kuhakikisha wanatimiza wajibu wao katika Malezi na makuzi kwa mtoto 

“Wanawake tuwe mstari wa mbele katika kupambana na vitendo vya ukatili ila hasa katika kujikwamua kiuchumi kwa kujishughulisha katika shughuli za maendeleo ili kupunguza vitendo hivyo ambavyo sababu kubwa ni uchumi” alisema Waziri Dkt. Gwajima

Aidha ameiasa jamii kutimiza wajibu wao kwa kutofumbia vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake na Makundi kwa kutoa taarifa na kuwa mstari wabele kutoa elimu kwa jamii kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kufanikisha azama hiyo ili kuwa na kizazi kilicho salama.

Akizungumza katika kikao hicho Naibu Waziri Mwanaidi Ali Khamis alisema kuwa Wizara inaungana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha inashirikiana na kutoa elimu kwa jamii kuhusu madhara ya ukatili katika jamii na kuwaalika wadau wengine kujitokeza kuonganisha nguvu pamoja na Serikali katika mapambano hayo.

” karibu wadau mbalimbali katika Wizara yetu tushauriane na kuweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha tunaikomboa Jamii dhidi ya vitendo vya ukatili unaendekea kutokea kila kukicha nchini ” alisema Naibu Waziri Mwanaidi

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt Zainab Chaula aliwashukuru Wanawake hao vinara na kuwahakikishia ushirikiano kwenye kuhakikisha nguvu kubwa inawekwa kutoa elimu kwa jamii ili iondokane na vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya Wanawake na Watoto.

Mwanamke kinara Dkt. Herieth Mkangaa alisema wako tayari kutoa elimu kwa jamii kuhusu madhara ya ukatili wa kijinsia kwa kushirikiana na Wizara kuhakikisha jamii inanufaika na eliu ya uchumi Afya Usawa wa Kijinsia na ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum inaendelea kukutana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha inaweka mikakati mbalimbali inayolenga kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

About the author

mzalendoeditor