Featured Kitaifa

MILIONI 61.4 ZATUMIKA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA KITUO CHA AFYA NDAGO

Written by mzalendoeditor

Mratibu wa Usafi wa Mazingira kutoka Wizara ya Afya, Ndugu Anyitike Mwakitalime akikagua miundombinu ya mfumo wa vyoo vinavyojengwa katika kituo cha Afya Ndago wilaya ya Iramba mkoani SingidaMuonekano wa mbele ujenzi wa vyoo vinavyojengwa katika kituo cha Afya Ndago wilaya ya Iramba mkoani SingidaMuonekano wa sehemu ya kunawia mikono katika vyoo vilivyojengwa katika kituo cha Afya Ndago wilaya ya Iramba mkoani Singida

Muonekano wa ujenzi wa choo cha walemavu katika kituo cha Afya Ndago wilaya ya Iramba mkoani Singida

**************

Na. WFA – IRAMBA- SINGIDA

Serikali kupitia wizara ya afya imetumia shilingi Milioni 61.4 kwa ajili ya ujenzi wa vyoo, miundombinu ya maji safi na taka pamoja na ujenzi wa kichomea taka katika kituo cha Afya Ndago, wilaya ya Iramba Mkoani Singida.

Kauli hiyo imetolewa na Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Ndago Dkt.Yasini Nyawangele wakati alipotembelewa na Timu ya Ufatiliaji wa utekelezaji wa Miradi ya Ujenzi wa vyoo, miundombinu ya maji safi na taka pamoja na usafi wa mazingira kutoka wizara ya Afya inayoongozwa na Ndg. Anyitike Mwakitalima.

Dkt. Nyawangele amesema kuwa utekelezaji wa mradi huo katika kituo cha afya Ndago umefikia asilimia 95 na wako mbioni kukamilisha hatua za mwisho ili mradi uanze kutoa huduma kwa wananchi wa tarafa na Kijiji cha Ndago.

“Mradi huu utakuwa msaada mkubwa katika kituo hiki kwani changamoto nyingi zitakuwa zimetatuliwa na hivyo maambukizi ya magonjwa yatapungua kulingana na ubora wa mradi huu utakavyotoa huduma hapa”. Ameeleza Dkt. Nyawangele.

Dkt. Nyawangele amesema mradi huo ukikamilika utafanya kituo hicho kuwa na matundu matano ya vyoo, mawili ya wanawake, mawili ya wanaume na moja kwa ajili ya walemavu.

Hivyo ametoa rai kwa wananchi wa Kijiji cha Ndago kuhakikisha wanautunza mradi huo ili kutoa huduma stahiki kama ilivyo tarajiwa.

Naye mmoja wa Wananchi wa Kijiji cha Ndago walionufaika na mradi huu katika ujenzi wa choo bora cha kudumu, Mzee Ismail Makala amesema kuwa anaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwahamasisha wananchi kujenga vyoo bora vya kudumu kwani itasaidia kupunguza maradhi katika familia zao.

About the author

mzalendoeditor