Uncategorized

UBALOZI WA UINGEREZA KUSHEREKEA MIAKA 70 YA UTAWALA WA MALIKIA ELIZABETH II NA MIAKA 60 YA URAFIKI WA TANZANIA NA UINGEREZA

Written by mzalendoeditor

Ubalozi wa Uingereza Dar es Salaam itasherekea Siku ya Kuzaliwa ya Malikia  Elizabeth II wa Uingereza Juni, 2 2022 pamoja na wageni waalikwa kuwa  Viongozi wa Serikali, Jumuiya ya Diplomasia nchini, Mashirikia yasiyo kuwa ya  Kiserikali, Sanaa, na Umoja wa Waingereza Tanzania. 

Sherehe za mwaka huu zina umuhimu wa kipekee kwani Uingereza inaadhimisha  miaka 96 ya Malikia Elizabeth na Jubilei ya miaka 70 ya Utawala wake. Malikia  ametawala kwa muda mrefu zaidi kuliko mfalme mwingine yeyote katika historia  ya Uingereza. 

Siku ya kuzaliwa ya Malikia ni wakati muhimu wa kusherehekea urafiki kati ya  Tanzania na Uingereza ambao mwaka huu inatimiza miaka 61 ya ushirikiano  baada ya uhuru.  

Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa  Afrika Mashariki, Liberata Mulamula. 

Kabla ya hafla hiyo, David Concar, Balozi wa Uingereza nchini Tanzania,  alisema: 

“Huu ni wakati maalum. Tunasherehekea miaka 70 ya utawala wa Malikia  na kujitolea kwake kwa Uingereza na Jumuiya ya Madola. Pia  tutasherehekea miongo sita ya urafiki ya baada ya uhuru kati ya Uingereza  na Tanzania na kuashiria mustakabali mzuri wa uhusiano huu wa kudumu  kati ya nchi hizi mbili za Jumuiya ya Madola. 

Katika sherehe hizi, Mwangaza wa Jubilei utawashwa tarehe 2 Juni 2022,  Bagamoyo na Moshi kama mojawapo ya vinara 1500 vitakavyomulika kote  Uingereza na Jumuiya ya Madola kama ishara ya umoja katika kusherehekea  Jubilei ya miaka 70. 

Kuelekea siku ya kuzaliwa kwa Malikia and Jubilei, ‘Wiki ya Waingereza’  (British Week) imefanyika hapa Dar es Salaam ikileta waingereza pamoja katika  sanaa, michezo na biashara. 

Nchini Uingereza, watu watasherehekea Jubilei kwa siku nne kuanzia Ijumaa na  kuwa na programu pana ya matukio ya umma ikijumuisha gwaride la Siku ya  Kuzaliwa, Ibada ya Shukrani na tamasha kuu la umma katika Jumba la  Buckingham. 

About the author

mzalendoeditor