Featured Kitaifa

WAZIRI MKUU APOKEA MAONI YA WAKAZI WA NGORONGORO

Written by mzalendoeditor

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea kutoka kwa Laigwnani Metui Ole Shaudo mapendekezo ya Wananchi wa Tarafa ya Ngorongoro kuhusu namna bora ya kudumisha  Hifadhi ya Ngorongoro wakati alipokutana na Mbunge wa Ngorongoro Emmanuel Shangay Malaigwani, Madiwani, Wenyeviti wa Vijiji pamoja na wawakilishi wa wanawake na Vijana kutoka wilaya ya Ngorongoro, ofisini kwa Waziri Mkuu,Mlimwa jijini Dodoma, 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea kutoka kwa Laigwnani Lawrance  Ngorisa mapendekezo ya Wananchi wa Tarafa za Loliondo na Sale  wilayani Ngorongoro kuhusu namna bora ya uhifadhi   wakati alipokutana na Mbunge wa Ngorongoro Emmanuel Shangay, Malaigwani, Madiwani, Wenyeviti wa Vijiji pamoja na wawakilishi wa wanawake na vijana wa tarafa za wilaya hiyo, ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma,

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na  Madiwani, wenyeviti wa Vijiji, Mbunge wa Ngorongoro Emmanuel Shangay   pamoja na wawakilishi wa vijana na wanawake wakati alipopokea mapendekezo ya wananchi wa Tarafa za Ngorongoro, Loliondo na Sale  wilayani Ngorongoro kuhusu namna bora ya uhifadhi  kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma,

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Malaigwanani kutoka Tarafa za Ngorongoro, Loliondo na Sale wilayani Ngorongoro baada  ya kupokea mapendekezo ya mwananchi kuhusu namna bora ya uhifadhi katika tarafa hizo, ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mei 25, 2022.  Kulia wake ni Mbunge wa Ngorongoro, Emmanuel Sangay na kushoto wake ni  Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Ngorongoro, Ndirango Ole Senge. 

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa wanawake  kutoka Tarafa za Ngorongoro, Loliondo na Sale wilayani Ngorongoro baada  ya kupokea mapendekezo ya mwananchi wa Tarafa hizo kuhusu namna bora ya uhifadhi katika tarafa hizo, ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mei 25, 2022. Kulia wake ni Mbunge wa Ngorongoro, Emmanuel Sangay na kushoto wake ni  Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Ngorongoro, Ndirango Ole Senge.

 Baadhi ya Madiwani, Wenyeviti wa Vijiji na wawakiizshi wa wanawake na vijana wa Tarafa  za Ngorongoro, Loliondo na Sare wilayani Ngorongoro wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipozungumza nao baada ya kupokea  mapendekezo ya Wananchi wa Tarafa  hizo kuhusu namna bora ya uhifadhi  kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma,

 (Picha  na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 ……………………………………….

 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa jana Mei 25, 2022 amepokea mapendekezo kutoka kwa wananchi wa Tarafa za Loliondo, Ngorongoro na Sale kuhusu namna bora ya kulinda uhifadhi wa maeneo hayo.

Maoni hayo yaliwasilishwa kwa Waziri Mkuu na wawakilishi wa wakazi wa wilaya hiyo wakiwemo Mbunge wa Ngorongoro Mhe. Emmanuel Shangai, Malaigwanani, Madiwani, wenyeviti wa vijiji, wawakilishi wa wanawake na vijana, ofisini kwake Mlimwa, Dodoma.

Baada ya kupokea mapendezo hayo, Waziri Mkuu aliwasisitiza wananchi hao waendelee kuiamini Serikali yao kwani haiwezi kuwa na mipango mibovu kwa wananchi wake. “Msisikilize maneno maneno ya watu wa pembeni.”

Akizungumzia kuhusu eneo la Msomera lililoko wilayani Handeni, Tanga ambako yanaandaliwa makazi kwa ajili ya kuwahamishia wakazi wa Ngorongoro waliokubali kuhama kwa hiari alisema ujenzi unandelea vizuri.

Waziri Mkuu alisema ujenzi wa nyumba za makazi 103 upo mbioni kukamilika na pia, Serikali imepanga kuongeza nyumba nyingine lengo likiwa ni kufikia nyumba 500 kwa ajili ya wakazi hao.

Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa alisema Serikali inaendelea kuimarisha sekta ya mifugo ili kuhakikisha wafugaji wote nchini wanapata tija kupitia shughuli hiyo.

About the author

mzalendoeditor