Kitaifa

MAJALIWA AWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA JENGO LA UFUNDI TOWER KATIKA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA

Written by mzalendoeditor

Waziri Mku  Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipoweka jiwe la msingi la jengo la Ufundi Tower katika Chuo cha Ufundi Arusha, Mei 24, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Saidi Issa ambaye ni Meneja wa Ktengo cha Uzalishaji, Chuo cha Ufundi Arusha kuhusu ujenzi wa Jengo la Ufundi  Tower wakati Waziri Mkuu alipoweka jiwe la msingi la jengo hilo jijini Arusha, Mei 24, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la jengo la Ufundi Tower katika  Chuo cha Ufundi Arusha, Mei 24, 2022.  Wa tatu kushoto ni  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Innocent Bashungwa, wa tatu kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,  Profesa Carolyne  Nombo na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella. Kushoto ni Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo na wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Zelot Stephene. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea  zawadi ya picha yake iliyochorwa na Mwanachuo wa Chuo cha Ufundi Arusha, Michael  Felix  (kulia) wakati alipoweka jiwe la msing  la ujenzi wa jengo la Ufundi Tower katika Chuo cha Ufundi Arusha, Mei 24,2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

Baadhi ya washiriki wa  hafla ya uwekaji wa  jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Ufundi Tower katika Chuo cha Ufundi Arusha  wakipiga makaofi kumkaribisha  mgeni rasmi  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowasili  kwenye viwanja vya Chuo hicho jijini Arusha, Mei 24, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Baadhi ya washiriki wa  hafla ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Ufundi Tower katika Chuo cha Ufundi Arusha  wakimsikiliza mgeni rasmi  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza kwenye viwanja vya Chuo hicho jijini Arusha, Mei 24, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

…………………………………………………
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA

WAZIRI mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema kuwa ameridhishwa na viwango vya ujenzi wa jengo la ufundi Tower katika chuo Cha ufundi Arusha (ATC) pamoja kusema kuwa  serikali inaendelea kufanya mapitio juu ya mkopo wa elimu ya juu kuona ni kwa namna gani mikopo hiyo itaweza kuwanufaisha na wanafunzi wanaosoma elimu ya kati.

Majaliwa ameyasema hayo leo Mei  24 wakati akiweka jiwe la msingi katika jengo la ufundi Tower ambapo alisema kuwa wamejikita sana kwenye shahada hivyo wakati umefika kuona ni namna gani  wataboresha  elimu ya kati ili vijana waweze kunufaika zaidi.
Ameeleza ameridika na ujenzi wa jengo hilo linalojuisha maabara, madarasa,pamoja na  clinic itayowahudumia watumishi, wanafunzi, na wananchi wa Arusha walio karibu na chuo hicho na kuahidi kuwa wataendelea kuleta fedha za ujenzi katika chuo hicho ili kupunguza changamoto ya mabweni.
Amefafanua serikali imetoa fedha za kutosha kwenye sekta ya elimu  kwanzia chekechea kwa wanafunzi wa kawaida wenye mahitaji maalum ambapo kwa sekondari wameanza kwa kujenga madarasa na sasa wanajenga mabweni ili kuondoa changamoto ya kutembea umbali mrefu kwa wanafunzi wa kike na wakiume.
Kwa upande wake Kaimu mkuu wa chuo cha ufundi Arusha Dkt Musa Chacha alisema kuwa ujenzi wa jengo hilo ulioanza Julai 2021 baada ya kupokea shilingi bilioni 1.449 kama ruzuku ya fedha za maendeleo kutoka serikali kuu kwaajili ya bweni la wasichana lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 428 ambapo lengo la mradi huo ni kuongeza fursa na idadi kwa wanafunzi wa kike.
Alisema chuo kilitenga bilioni 1.036 ya mapato yake ya ndani mwaka wa fedha 2021/2022 ili kujenga cliniki ya tiba inayolenga kuboresha utoaji wa mafunzo kwa wanafunzi wanaosoma programu ya vifaa tiba ambapo jengo la ghorofa tatu na sakafu moja ya chini lenye maabara, madarasa, ofisi na stoo ambalo limepewa jina la Ufundi Tower.
Kwa upande wake katibu mkuu wizara ya Elimu sayansi na teknolojia …. Alisema kuwa  kupitia ushawishi wa Rais Samia Suluhu wameweza kupata fedha kwaajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya kuboreshe miundombinu ya kufundishia ambapo wizara ya Elimu ilipata bilioni 64.9 kwaajili ya kukamisha miradi mbalimbali kupitia fedha za UVIKO-19.

About the author

mzalendoeditor