Featured Kitaifa

CRDB BAADA YA KUPATA MAFANIKIO MAKUBWA 2021 SASA YAJA NA MPANGO WA KUANGALIA FURSA MPYA.

Written by mzalendoeditor

NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA

Taasisi ya fedha ya CRDB baada ya kupata mafanikio makubwa 2021 ya bilioni 268 sasa imejipanga kuangalia fursa mpya na kuhakikisha wanaendelea kutoa bidhaa zinazohitajika na wateja.
Hayo yameelezwa na mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo Abdulmajid Nsekela wakati akiwasilisha taarifa  ya Benki hiyo ya mwaka uliosha 2021 katika mkutano mkuu wa 27 wa wanahisa kwa mwaka 2022 ambapo alisema kuwa kwa muda uliobaki wa 2022 watahakikisha huduma zao zinamfikia kila mteja kwa kutoa bidhaa zinazohitajika.
Nsekela alisema kuwa  pia wataendelea kuhakikisha wanakuwa Benki inayohudumia wateja kwa haraka nchini  (Benki fasta) lakini pia kuendelea kuwa makini na athari zinazoweza kujitokeza kwa kuweka miundo mizuri ya viashiria vya majanga.
Akiendelea kuelezea mafanikio alisema kuwa kwa mwaka 2021 wameonheza mahusiani na NHIF kwa kuwa wakwanza kutoa bima afya kwa wakulima inayotolewa bure alafu malipo yanafanyika baada ya mkulima kuvuna  ambapo programu hiyo imeifanya  CRDB kuwa benki ya kipekee nchini.
“Pia tumekuwa na mahusiani ya karibu na wajasiriamali na wafanyabiashara hasa akina mama kwa kuanzisha huduma mahususi kwaajili yao pamoja na asilimia 93 ya huduma zetu kufanyika nje ya matawi  kutokana na uwezeshwaji mkubwa wa teknolojia, pamoja na kupata tuzo mbalimbali zinazofanya benki kuzidi kuheshimika,” Alisema Nsekela.
Kwa upande  wake mkurugenzi wa fedha wa Benki hiyo Fredrick Nshekenabo Alieleza kuwa mafanikio hayo pia yamechangia na mapato yasiyokuwa na riba na kukuza midhania ya Benki pamoja na kuendelea na mkakati wa kudhibiti gharama za uendeshaji kutoka asilimia 61 Hadi kufikia asilimia 55.
“Mikopo imekua kwa asilimia 28 kwa wateja wadogo kwa asilimia 59 na wakubwa kwa asilimia 40.8 ambapo Hadi kufunga mwaka mikopo chechefu ilishuka na kufikia 3.3%  huku kiasi Cha fedha kilichopo kama mtaji kikiwa ni Trilioni 9.4,” Alisema.
Naye Mkurugenzi mstaafu wa Benki hiyo Dkt Charles Kimei  ambaye pia ni mbunge wa Jimbo Vunjo alisema  anawapongeza viongozi kwasababu pamoja na uwepo wa COVID- 19 wamepata faida kubwa tofauti na makampuni mengi ambapo pia ameshauri benki  kuhusiana na kasi ya ukuaji, kuwa makini kwani ukuaji mkubwa unaogopesha.
“Faida inapokuwa kubwa inafurahisha lakini pia tujue kuwa watu pengine wamelipa tozo kubwa zaidi kwahiyo kwasababu sisi ni benki kubwa tuangalie namna ya kuendesha hoja ya kujaribu kupunguzaji tozo wanazotozwa watu pamoja na riba,”  Alisema Dkt Kimei.
“Gawiwo tunalolipata ni zuri na kila mwanahisa anatamani kupata faida kubwa lakini tuweke usawa tusitake kupata faida kubwa, tuweke tozo ambazo zitakuwa na usawa,”Alisema .

About the author

mzalendoeditor