Featured Kitaifa

MAWAZIRI AFRIKA MASHARIKI WAKUBALIANA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Written by mzalendoeditor

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akizungumza wakati wa Mkutano wa 8 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Mazingira na Maliasili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika katika Ukumbi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja akizungumza wakati wa Mkutano wa 8 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Mazingira na Maliasili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika katika Ukumbi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha.

Waziri wa Mazingira na Maliasili wa Kenya Mhe. Keriako Tobiko akiongoza Mkutano wa 8 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Mazingira na Maliasili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika katika Ukumbi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha.

Ujumbe kutoka Tanzania wakishiriki Mkutano wa 8 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Mazingira na Maliasili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika katika Ukumbi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha.

Mawaziri, Makatibu wakuu na viongozi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa 8 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Mazingira na Maliasili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika katika Ukumbi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha.

(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)

………………………………………………

Mawaziri wa Sekta ya Mazingira na Maliasili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wamekubaliana katika uhifadhi endelevu na usimamzi wa mazingira na maliasili zilizopo katika eneo hilo. 

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Khamis Hamza Khamis aliposhiriki Mkutano wa 8 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Mazingira na Maliasili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo Mhe. Khamis alisema pamoja na mambo mbalimbali wamepata fursa ya kujadili na kuwekeana mikakati ya uhifadhi wa mazingira.

Alisema eneo la Afrika Mashariki linakabiliwa na uharibu wa mazingira hivyo wamejadiliana namna bora ya kushirikiana katika utunzaji wa vyanzo vya maji pamoja, kushughulikia changamoto ya uchafuzi wa mazingira kutokana na plastiki.

“Tumekutana hapa kujadiliana na kukubaliana kuelimisha wananchi wetu kuhusu masuala mbalimbali yakiwemo namna bora ya kuepana taalumu (kuelimishana) kuhusu matumizi bora ya ardhi sasa hivi tunaona migogori mingi na pia watu wanafanya uharibu wa mazingira kupitia ardhi,” alisema Naibu Waziri Chilo.

Aidha, aliongeza kuwa hivi sasa tunatekeleza miradi mikubwa ya mazingira ikiwemo ya hewa ya ukaa ambayo inaleta faida kwa Serikali zetu na wananchi wake kwa ujumla hivyo wanapaswa kufahamu.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja alisema mkutano huo ni fursa ya kujadili mikakati ya kuhakikisha usimamizi mzuri wa mazingira na maliasili katika ukanda eneo hilo.

Pia, Naibu Waziri Masanja aliongeza kuwa mkutano huo umejadili mikakati ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi zinazoathiri maendeleo ya kijamii miongoni mwa wananchi hao.

Waziri wa Mazingira na Maliasili wa Kenya Mhe. Keriako Tobiko ambaye aliongoza mkutano huo alisema changamoto ya uharibifu wa mazingira bado inakabili ukanda wa Afrika Mashariki na hivyo kuhatarisha maisha.

Alisema kuwa kutokana na hilo ni jukumu la nchi wanachama kushirikiana kwa pamoja katika kuhakikisha changamoto hiyo ya uharibifu wa mazingira inafanyiwa kazi na kuondoshwa.

Naye Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Peter Mathuki alisema baada ya kuhitimishwa kwa mkutano kama nchi wanachama wamepanga kutekeleza yale yote waliyokubaliana.

Alisema katika changamoto kubwa ya mabadiliko ya tabianchi mawaziri wana wajibu wa kuhakikisha wananchi wanapata manufaa ya kile kilichokubalika katika mkutano huo kuhusu uhifadhi wa mazingira.

Mkutano huo umeshirikika nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki zikiwemo Tanzania, Uganda, Kenya, Sudan Kusini, Burundi na Rwanda ambapo Tanzania mbali ya kuwakilishwa na mawaziri wa Sekta ya Mazingira pia Waziri wa Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo wa Zanzibar Mhe. Shamata Shame Khamis na wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais.

About the author

mzalendoeditor