Featured Kitaifa

MBUNGE MTATURU AIBANA SERIKALI

Written by mzalendoeditor

MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameihoji serikali kuwa ni lini wananchi wa Tarafa ya Mungaa watapata umeme kama ilivyo dhamira yake ya kufikisha umeme katika vijiji vyote.

Akiuliza swali la nyongeza Mei 19,2022,Bungeni Jijini Dodoma,Mtaturu amesema katika Tarafa hiyo hakuna kijiji hata kimoja chenye umeme.

“Juhudi zilifanyika na Kata nne zimeshawekewa nguzo leo ni mwezi wanne unaenda watano,ni lini sasa mkandarasi atarudi kwenda kuweka nyaya na transfoma ili wananchi waweze kupata umeme wakati wengine wanasubiri nguzo zilizobakia,”amehoji Mtaturu.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Nishati Stephen Byabato amesema kulitokea changamoto ya ongezeko la bei hasa kwenye bidhaa zinazotumika kutengeneza transfoma .

“Katika kujadili tatizo hili na kulitatua itachukua muda kidogo lakini tunakaribia kulimaliza,na tunaamini mwisho wa mwezi huu basi habari ya kuvuta waya,kufunga transfoma na mengine yanaendelea kwenye maeneo ambayo tayari nguzo zilishasimamishwa,”amesema.

Amewaelekeza wakandarasi wote nchini kuhakikisha yale maeneo ambayo nguzo hazijasimama, kazi zisizohusika na ongezeko la bei ziendelee kufanyika wakati kazi nyingine zikiendelea kukamilika ili kuhakikisha umeme unafika kwa wakati.

About the author

mzalendoeditor