Featured Kitaifa

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA  NDG SAMIA SULUHU HASSAN ATEMBELEA OFISI ZA CCM MKOA WA TABORA

Written by mzalendoeditor
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg Samia Suluhu Hassan , Akisain Vitabu Vya Wageni katika Ofisi ya CCM Mkoa wa Tabora. Mapema leo asubuh 
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg Samia Suluhu Hassan , akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Tabora Mapema leo asubuhi 
Wajumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Tabora wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg Samia Suluhu Hassan alipokuwa akizungumza nao mapema leo asubuhi Mei 18, 2022.
………………………………
 
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan leo Jumatano tarehe 18 Mei, 2022 ametembelea ofisi za Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora ambapo alipata nafasi ya kusaini vitabu vya wageni, kukutana na kufanya mazungumzo na kamati ya siasa ya mkoa huo.
 
Pamoja na mambo mengine Mwenyekiti wa CCM Taifa alipokea taarifa ya mwenendo wa uchaguzi wa ndani ya chama unaoendelea na kujadiliana masuala mbalimbali yenye ustawi na CCM na wananchi wa Tabora kwa ujumla.
 
Awali Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora Ndg Hassan wakasuvi akimkaribisha Ndg Samia Suluhu Hassan alimueleza kuwa Chama Cha Mapinduzi mkoani Tabora na wananchi kwa ujumla wanaridhishwa na utendaji wa serikali anayoiongoza katika kuimarisha utoaji huduma, ujenzi wa miundombinu na ukuzaji wa uchumi kwa wananchi mkoani humo ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.
 
“Nimekuwa mwanachama wa chama hiki na kiongozi kwa miaka 25 lakini tukio la Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutembelea ofisi za chama chetu na kuzungumza na viongozi wake hili ni tukio la kwanza kwa mkoa wa Tabora. Haya ni mahusiano mazuri baina ya chama na serikali, tunakushukuru sana na tunakukaribisha Tabora.” alisema  Ndugu Mwakasubi.
 
Rais Samia Suluhu Hassan yupo mkoani Tabora kwa ziara ya kikazi ya siku tatu aliyoianza tarehe 17 Mei, 2022 na ataihitimisha tarehe 19 Mei, 2022 kwa kuwahutubia wananchi wa mkoa wa Tabora katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi. 
 
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
 
Shaka Hamdu Shaka
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa
Itikadi na uenezi

About the author

mzalendoeditor