Featured Kitaifa

WANAFUNZI 10008 WAKABIDHIWA TAULO ZA KIKE WILAYANI MISUNGWI.

Written by mzalendoeditor
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel akizungumza kwenye hafla ya ugawaji wa taulo za kike kwa wanafunzi wa shule za Sekondari zilizopo Wilayani Misungwi.
Sabrina yahya (mwenye ushungi) mwanafunzi kutoka Shule ya Sekondari Misungwi akisoma risala kwenye hafla ya ugawaji wa taulo za kike kwa wanafunzi 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Dowe Care Victor Zhang akizungumza wakati wa hafla ya ugawaji wa taulo za kike kwa wanafunzi wa shule za sekondari zilizopo Wilayani Misungwi 
Balozi wa Soft care Zarinah Hassan (Katika) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel wakikabidhi boksi lenye taulo za kike kwa mwanafunzi.
Zarinah Hassan balozi wa Doweicare Technology Limited akizungumza kwenye hafla ya ugawaji wa taulo za kike iliyofanyika katika viwanja vya shule ya Sekondari Misungwi 
……………………………………….
Na Hellen Mtereko, Misungwi
Wanafunzi wanaosoma shule mbalimbali za sekondari katika Wilaya ya Misungi Jijini Mwanza wamepewa taulo za kike (Pedi) ili kuwanusuru kukosa vipindi vya masomo darasani kwa kutohudhuria shuleni pindi wanapoingia kwenye siku zao za hedhi.
Taulo hizo zimetolewa na Kampuni ya Doweicare Technology Limited kwa lengo la kuunga juhudi za Serikali za kumuwezesha mtoto wa kike kusoma na kukaa kwa uhuru pindi anapokuwa kwenye hedhi.
Hafla ya ugawaji wa taulo hizo kwa shule 32 za Serikali zilizopo katika Wilaya ya Misungi imefanyika leo May 14,2022 katika viwanja vya shule ya Sekondari Misungwi.
Akizungumza kwenye hafla ya ugawaji wa  taulo hizo Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Victor Zhang, amesema kuwa kwa Mkoa wa Mwanza ni mara ya kwanza kurejesha katika Jamii kwa kuchangia bidhaa za taulo za kike kwa wahitaji ambapo leo  wamechangia bidhaa hizo zenye thamani ya milioni 13 kwa wanafunzi   wa Misungwi.
Zhang amesema kuwa dhamira yao kubwa ni kuboresha hali ya kimaisha za mabinti kwa kuwapa bidhaa ambazo zitawasaidia kuwastiri sanjari na kuchangia uchumi wa nchi.
Kwa upande wake balozi wa Kampuni hiyo Zarinah Hassan, amesema kuwa wazazi wanapokuwa wananunua mahitaji ya wanafunzi wa kike wawe wanakumbuka pia kununua taulo za kike na wazipe kipaumbile cha kwanza ili wanapopata hedhi wakiwa shuleni waweze kujistiri vizuri na kuendelea na masomo yao kwa amani.
Akizungumza kwa niaba ya Afisa elimu wa Wilaya ya Misungwi,Afisa elimu taaluma Sekondari Selema Ikowe, ameushukuru uongozi wa kampuni ya Doweicare Technology Limited kwa kutoa msaada huo kwa watoto wa kike kwani Watoto wengi  wanatokea katika mazingira magumu hali inayopekekea kushindwa kupata uwezo wa kununua taulo hizo kwaajili ya kujihifadhi.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Veronica Kessy, amesema kuwa taulo hizo zitawasaidia watoto kuchochea maendeleo ya taaluma yao kwani wataweza kuhudhuria darasani wakati wote na watakuwa huru.
Akisoma risala iliyoandaliwa na wanafunzi wa shule hizo Sabrina yahya kutoka shule ya Sekondari Misungwi wamesema kuwa taulo za kike zinawasaidia kujiamini na kujipa thamani na inamsaidia mwanafunzi kutokukatisha masomo yake pindi anapopata hedhi.
Aidha,wameomba kuwepo na mfumo wa huduma maalumu ya hedhi shuleni ikiwemo chumba maalumu cha kubadilishia taulo za kike, dawa za kupunguza maumivu na msaada wa kisaikolojoa kwa wasichana walioko kwenye hedhi.
Akijibu risala iliyoandaliwa na wanafunzi hao Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel, amesema kuwa hedhi salama ni muhimu kwa afya, maendeleo na utu wa msichana na mwanamke kuanzia shule za msingi,Sekondari,vyuo pamoja na walioko nyumbani wote wanahitaji upatikanaji wa huduma za hedhi iliyo salama bila kuwa na vikwazo.
Amesema kuwa ni dhahili kwamba wasichana na wanawake katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania wanakabiliwa na changamoto ya mazingira yasiyo rafiki wakati wa hedhi hususani upatikanaji wa maji safi na salama vyoo bora na chumba cha kubadilishia taulo za kike.
“Nitoe wito kwa wadau wa elimu kuendelea kuwa na moyo wa kujitolea kuwasaidia wasichana kupata taulo za kike pamoja na kuwatengenezea mazingira mazuri ya hedhi salama ili kuweza kuepukana na magonjwa mbalimbali”,amesema Gabriel

About the author

mzalendoeditor