Featured Kitaifa

NDEJEMBI ATAKA WAHITIMU WA MAFUNZO YA UONGOZI KUSIMAMIA RASILIAMALIWATU NA FEDHA

Written by mzalendoeditor

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na wahitimu wa     Astashada na Stashahada ya Uzamili ya Uongozi wakati wa mahafali ya tano ya Taasisi ya UONGOZI yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Wahitimu wa Astashada na Stashahada ya Uzamili ya Uongozi wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi alipokuwa akizungumza nao wakati wa mahafali ya tano ya Taasisi ya UONGOZI yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Kiongozi wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Mhandisi Zena Ahmed Said akitoa akihimiza uwajibikaji kwa Wahitimu wa Astashada na Stashahada ya Uzamili ya Uongozi wakati wa mahafali ya tano ya Taasisi ya UONGOZI yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya UONGOZI, Balozi Ombeni Sefue akitoa nasaha kwa Wahitimu wa Astashada na Stashahada ya Uzamili ya Uongozi wakati wa mahafali ya tano ya Taasisi ya UONGOZI yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi kuzungumza na Wahitimu wa Astashada na Stashahada ya Uzamili ya Uongozi wakati wa mahafali ya tano ya Taasisi ya UONGOZI yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI, Bw. Kadari Singo akielezea maudhui ya mafunzo yanayotolewa na taasisi yake wakati mahafali ya tano ya Taasisi ya UONGOZI yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Aalto cha Finland, Dkt. Pekka Mattila akiwahimiza Wahitimu wa Astashada na Stashahada ya Uzamili ya Uongozi kutumia ujuzi walioupata katika utekelezaji wa majukumu yao wakati wa mahafali ya tano ya Taasisi ya UONGOZI yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Mhitimu wa Stashahada ya Uzamili ya uongozi, Bi. Rabia Mohammed akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Wahitimu wa Astashada na Stashahada ya Uzamili ya Uongozi wakati wa mahafali ya tano ya Taasisi ya UONGOZI yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akimtunuku cheti cha Stashahada ya Uzamili ya Uongozi Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Jokate Mwegelo wakati wa mahafali ya tano ya Taasisi ya UONGOZI yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Wahitimu wakionyesha vyeti walivyotunukiwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi wakati wa mahafali ya tano ya Taasisi ya UONGOZI yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

………………………………………………….

Na. James K. Mwanamyoto-Dar es Salaam

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka Watumishi wa Umma waliohitimu mafunzo ya uongozi katika Taasisi ya UONGOZI kuhakikisha wanaitumia vizuri elimu waliyoipata katika kusimamia rasilimaliwatu na rasilimali fedha kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Mhe. Ndejembi ametoa nasaha hizo jijini Dar es Salaam kwa wahitimu wa Astashada na Stashahada ya Uzamili ya Uongozi wa Taasisi ya UONGOZI, katika Mahafali yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City.

Mhe. Ndejembi amesema, Serikali inatarajia kuona uongozi wa kimkakati kwa wahitimu hao hususani kwenye eneo la usimamizi wa rasilimaliwatu na fedha ili taifa liweze kunufaika na elimu waliyoipata.

Ameongeza kuwa, Serikali inatarajia kuona maboresho makubwa katika nyanja ya mawasiliano na mahusiano miongoni mwao na baina yao na wadau wa maendeleo kwa ajili ya mustakabali wa maendeleo ya taifa. 

“Mmefundishwa uzingatiaji wa maadili, kuongoza kwa kuzingatia misingi ya utawala bora pamoja na kuelezwa athari za rushwa katika kutekeleza majukumu yenu, hivyo tunategemea mtakaporudi katika vituo vyenu vya kazi mtakuwa watumishi bora na waadilifu kiutendaji”, Mhe. Ndejembi amesisitiza.

Naibu Waziri Ndejembi ameeleza kuwa, mafunzo ya uongozi waliyopatiwa wahitimu hao ni sehemu ya kuwajengea uwezo wa kusimamia rasilimali za nchi kikamilifu kwa maendeleo ya taifa.

Mhe. Ndejembi amefafanua kuwa, kazi ya kuwajengea uwezo kiutendaji iliyofanywa na Taasisi ya UONGOZI kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Aalto cha Finland inaunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita katika kutekeleza mpango wa maendeleo, hivyo ameipongeza Taasisi ya UONGOZI na chuo hicho kwa kuwajengea uwezo viongozi hao.

“Ni matumaini yangu kuwa mafunzo haya mliyoyapata yatawawezesha kukuza na kuimarisha uongozi na utawala bora wenye kuzingatia haki, na uwajibikaji katika maeneo yenu ya kazi, na kuongeza kuwa ni vema wakatambua kwamba kiongozi mzuri ni yule anayewajibika na kutekeleza majukumu yake bila kushurutishwa”, Mhe. Ndejembi amehimiza.

Aidha, Mhe. Ndejembi amewataka viongozi katika Wizara, Idara na Taasisi nyingine za Umma na binafsi kutenga fedha za mafunzo kwa ajili ya kuendeleza viongozi katika Taasisi ya UONGOZI ili waweze kuongeza weledi na kuwa chachu ya maendeleo katika taifa. 

Akizungumza kwa niaba ya wahitimu, Bi. Rabia Mohammed amesema kwa hakika wamepata elimu na kujifunza mengi ya kiuongozi na si kwa nadharia tu bali kwa vitendo, hivyo wanaahidi kuyaishi na kuyatendea kazi kwa ajili ya masilahi mapana ya taifa.

Bi. Rabia ametoa wito kwa viongozi wote wa umma na taasisi binafsi kuzingatia maadili, nidhamu na uchapakazi na kwa upande wao wanaahidi kuwa mfano wa kuigwa katika uzingatiaji wa maadili, nidhamu na uchapakazi.

Jumla ya viongozi 117 kutoka taasisi za umma na sekta binafsi wamehitimu mafunzo ya uongozi yanayotolewa na Taasisi ya UONGOZI na kutunikiwa vyeti kwa ngazi ya Astashahada na Stashahada ya Uzamili ya uongozi. 

About the author

mzalendoeditor