Kitaifa

MAKAMU WA RAIS KUZINDUA ROYAL TOUR JIJINI DODOMA

Written by mzalendoeditor

MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 13,2022 wakati akitangaza ujio wa uzinduzi wa Filamu ya Royal Tour utakaofanyika siku ya Jumapili Mei 15,2022 kuanzia saa 12:00 Jioni katika Ukumbi wa Mikutano wa JK Conversion Center jijini Dodoma.

MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari leo Mei 13,2022 wakati akitangaza ujio wa uzinduzi wa Filamu ya Royal Tour utakaofanyika siku ya Jumapili Mei 15,2022 kuanzia saa 12:00 Jioni katika Ukumbi wa Mikutano wa JK Conversion Center jijini Dodoma.

………………………………………………

Na Alex Sonna-DODOMA

MAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Philip Mpango,anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa filamu ya Royal Tour jijini Dodoma.

MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka ametoa taarifa ya ujio wa uzinduzi wa Royal Tour  leo Mei 13,2022 jijini Dodoma  wakati akizungumza na waandishi wa habari,amesema kuwa uzinduzi wa filamu hiyo utafanyika siku ya Jumapili Mei 15,2022  kuanzia saa 12:00 Jioni katika Ukumbi wa Mikutano wa JK Conversion Center.

RC Mtaka amesema kuwa ujio huo ni baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuzindua filamu hiyo nchini Marekani na maeneo mengine nchini.

Aidha ameeleza kuwa uzinduzi huo utahusisha matukio mbalimbali ikiwemo maonyesho ya utamaduni wa asili ya wenyeji wa mkoa wa Dodoma,mazao ya zabibu na ngoma za kitamaduni za kigogo na kirangi.

“Maandalizi yamekamilika kutakuwa jogging na burudani itayobebwa na utamaduni wa Dodoma ngoma za kigogo na kirangi,milango iko wazi kwa watakaopenda kujiunga na tukio hili,”amesema RC Mtaka

Mtaka amezitaka sekta binafsi,wafanyabiashara na Wadau wa maendeleo kushiriki kwenye tuki hilo ili kukuza sekta ya utaalii na kufungua mipango ya sekta ya uchumi

“Zao la zabibu linaongeza thamana ya yake kutoka kwenye wine kwenye mvinyo, tutakuwa na maonyesho ya mazao ya zabibu pia,”amesema

Amesema kuwa Ofisi yake imetoa fursa kwa baadhi ya Wilaya kuangalia tukio hili kupitia vyombo vya habari na utaratibu wote umekamilika.

Ikumbukwe kuwa mbali na Dodoma filamu ya Royal Tour ilianza kuzinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huko nchini Marekani na hatimae jijini Arusha ,Zanzibar na Dar es Salaam.

About the author

mzalendoeditor