Featured Kitaifa

WAUGUZI BADILIKENI KATIKA UTOAJI HUDUMA ZENU

Written by mzalendoeditor

Rais wa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA) akifunga Kikao kazi cha Viongozi wauguzi kilichofanyika leo mkoani Kilimanjaro.

Muuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Elianeth Kiteni akiwasilisha mada katika kikao kazi cha Viongozi wauguzi kilichofanyika leo Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Baadhi ya Viongozi wauguzi wakifatilia mijadala mbalimbalia katika kikao kazi cha viongozi wauguzi kilichofanyika leo Moshi- Kilimanjaro.

Baadhi ya Viongozi wauguzi wakifatilia mijadala mbalimbalia katika kikao kazi cha viongozi wauguzi kilichofanyika leo Moshi- Kilimanjaro.

Baadhi ya Viongozi wauguzi wakifatilia mijadala mbalimbalia katika kikao kazi cha viongozi wauguzi kilichofanyika leo Moshi- Kilimanjaro.

Mwenyekiti wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Prof. Lilian Mselle (Kwanza Kulia) akijadiliana na Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Agness Mtawa leo wakati wa kikao kazi cha viongozi wauuguzi Mkoani Kilimanjaro.

Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Agness Mtawa akiwasilisha mada katika kikao kazi cha Viongozi wauguzi kilichofanyika leo Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Muuguzi Mkuu wa Serikali, Bi. Ziada Sellaha akifungua Kikao kazi cha Viongozi wauguzi kilichofanyika leo mkoani Kilimanjaro

………………………………

Na. WAF- KILIMANJARO
Wauguzi nchini wametakiwa kubadili fikra zao katika utendaji kazi ili kuleta ubora wa huduma kwa wateja wanaowahudumia katika vituo vyao vya kazi.

Wito huo umetolewa leo na Muuguzi Mkuu wa Serikali, Bi Ziada Sellah Mkoani Kilimajaro wakati wa ufunguzi wa Kikao kazi cha Viongozi wauguzi ambapo amesema wauguzi wanatakiwa kuona wagonjwa kama wafalme wakati wa kuwahudumia ili wakawe mabalozi wao katika kazi wanazofanya kazini.

Bi. Ziada Amesema kuwa mtu yeyote bila kubadili fikra hata kama anauelewa wakutosha hawezi kuonekana kama muuguzi au mkunga anayeka wodini na kutoa huduma.
“Ili kufikia maleng yetu katika kuhudumia wananchi lazima kutoa huduma kwa usawa kama tulivyofundishwa katika maadili ya kazi na bila kuangalia unayemuhudumia ni nani kwani kesho utahitaji huduma ya muuguzi mwenzako”, amesisitiza Bi. Ziada

“Wauguzi mnapotekeleza majukumu yenu mvae viatu vya mteja unayemuhudumia kwa wakati huo alafu piga picha ni ndugu yako yuko mbali nawe anahudumiwa na mtu mwingine” amesema Bi. Ziada

Bi. Ziada amesema kuwa Wauguzi Viongozi wanaposimamia wauguzi wenzao wakumbuke kusimamia maswala mazima ya huduma kwa mteja, kubadili fikra na kusimamia maadili ya kazi ili kuboresha utendaji kazi na viongozi wawe mfano wa kuigwa.

“Niwasii sana katika kuelekea siku ya wauguzi Duniani inayofanyika 12 Mei mwaka huu hapa mkoani Kilimanjaro twende tukabadilike na tusimamie wanafunzi wanaokuja kufanya masomo yao kwa vitendo kufata maadili ya uuguzi kama tulivyofundishwa”ametoa rai Bi. Ziada.

Kwa upande wake Rais wa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA), Alexander Baluhya amesema lengo la kikao kazi hicho ni kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili taaluma na kuangalia namna ambavyo wanaweza kuzitatua ili kuimarisha ushirikiano katika maswala mazima ya kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

“Katika kuelekea siku ya Wauguzi Duniani Tarehe 12 Mei,2022 Kitaifa maadhimisho haya yatafanyika Moshi- Kilimanjaro ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majali” ameeleza Baluhya

Baluhya amesema kuwa Kauli mbiu ya Mwaka huu ni “Wauguzi ni sauti inayoongoza wekeza na Heshimu haki za watu kwa maboresho ya huduma za afya kwa wote”.

Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Agnes Mtawa amewakumbusha watalaamu hao kujitambua kwa kuwasilisha taarifa zao kwa baraza kila baada ya kutoka masomoni ili kuwa na taarfa sahihi za muuguzi husika.

Mwenyekiti wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Prof. Lilian Mselle amewataka wataalamu hao kujitathimini katika utendaji kazi wao ili kuleta ubora na ufanisi katika kazi ya uuguzi wodi.

“Tukifanya kazi zetu kwa welidi changamoto ndogondogo tunazotupiwa wauguzi azitakuwepo basi tufanye kazi kwa weledi na kufata maadili ya kazi yanavyo taka”, amesisitiza Prof. Lilian.

Naye Muuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Elianeth Kiteni amesema kuwa wauguzi ni uti wa mgongo katika mfumo mzima wa huduma za afya akibainisha kwamba ili kufikia adhima hiyo wanapaswa kufuata miiko ya uuguzi katika kutekeleza majukumu yao kwa ufasaha na kuongeza tija katika utoaji huduma kwa wananchi wanao nufaika na huduma za afya.

About the author

mzalendoeditor