Featured Kitaifa

KONGAMANO LA AIESEC LAFANYIKA CHUO KIKUU CHA MZUMBE

Written by mzalendoeditor
Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe,kampasi ya Morogoro wakifuatilia mada wakati wa kongamano hilo.

*
Kongamano la kuwajengea Wanafunzi wa vyuo vikuu lililoandaliwa na taasisi ya AIESEC tawi la Tanzania na kudhaminiwa na Kampuni ya Madini ya Barrick, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali limefanyika katika Chuo Kikuu cha Mzumbe –Morogoro, ambapo wataalamu mbalimbali walitoa mada za kuwajengea uwezo Wanafunzi kusoma kwa bidii na kuzidi kuwa wabunifu ili waweze kwenda sambamba na mabadiliko ya kiteknolojia na kidigitali ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali zinazojitokeza na kuwa na uwezo wa kujiajiri.

 

Afisa mwajiri wa kampuni ya Barrick, Alfa Rashid (kushoto) akibadilishana mawazo na Watendaji kutoka taasisi ya AIESEC.

 

Mhadhiri wa Chuo kikuu Mzumbe Dkt. Albogasti Mkabila, akibadilishana mawazo na Diwani wa kata ya Mzumbe, Godfrey Fransis, wakati wa kongamano.
Baadhi ya Wanafunzi wakipiga picha ya pamoja na watoa mada,waandaaji na wawakilishi wa makampuni yaliyofadhili kongamano hilo.

About the author

mzalendoeditor