Featured Kitaifa

HALMASHAURI 144 ZANUFAIKA NA MEWAKA

Written by mzalendoeditor

Asila Twaha – Bukoba Dc

Halmashauri 144 kati ya 184 zilizoko Tanzania bara zimenufaika na mafunzo endelevu ha Walimu Kazini (MEWAKA) ili kuwajenge uwezo Walimu katika utoaji wa elimu bora na kuendana na uboreshaji wa Elimu unaoendelea nchi nzima.

Mratibu wa Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini(MEWAKA) Cosmas Mahenge amesema, mpaka sasa Walimu kutoka Halmashauri takribani 122 zimeshapatiwa mafunzo hayo na sasa wanamaliza katika Kanda ya Ziwa na Magharibi.

Mahenge ameleeleza hayo tarehe 9 Mei, 2022 Mkoani Kagera wakati akiongea na walimu wakati wa kufungua mafunzo hayo Ana kueleza kuwa mafunzo hayo yamelenga walimu wa shule ya awali na msingi lengo ni kuwaendeleza kitaalam na kitaaluma kuwapa mbinu za ujifunzaji na ufundishaji na jinsi ya kuweza kutatua changamoto wanapokuwa katika vituo vya kazi.

Amesema mafunzo ya MEWAKA mbali ya kujifunza mbinu za ujifunzaji na ufundishaji yatamsaidia mwalimu kuendana na mbabiliko yanayotokea katika elimu na jamii tunayoishi na walimu ni lazima wabadilike.

tunaamini umahiri na njia bora ya mwalimu anayotumia ndio inaenda kumsaidia mwanafunzi awe bora zaidi.

Aidha, amesema baada ya mafunzo hayo kumalizika takribani walimu 26,657 watakuwa wamepata mafunzo na Halmashauri 144.

“Niwaombe walimu pamoja na kuendelea kwamafunzo haya yasiathiri ratiba za kufundishia madarasani hivyo kila mmoja asingatie sheria, kanuni na taratibu za mafunzo na tuwe mabolozi wazuri kwa walimu wenzetu na wanafunzi wetu tunaowasimamia” amsesema Cosmas

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Wawezeshaji wa MEWAKA Bw. Ferdinand Mlandali amesema, maufunzo yatamsaidia mwalimu kujifunza na kuendana na mabadiliko ya sekta ya elimu.

Walimu watawezeshwa kujua njia za kufunza ikiwemo mitaala na kumsaidia kuendana na karne ya 21 ikiwa ni pamoja na mawasiliano, ubunifu, namna ya kujifunza kwa pamoja ili kuwasaidia wanafunzi hata wanapo rudi nyumbani waweza kufanya vizuri.

Aidha, amesema mafunzo haya pia yatamuwezesha mwalimu kujua njia ya “learning management system” na kuweza kujifunza kutumia maktaba mtandao kwa kuweza kupakua/kupata na materials mbalimbali.

Naye Sista Felista Pamerace(Mwl.Shule ya Msingi Mwemage) amesema, wapo tayari kujifunza na kuelekezwa na kuwa mabalozi wazuri wa walimu wenzao kwa kuwaelekeza na kwa wanafunzi kuweza kuwafundisha.

“Tuliomba muda mrefu Serikali iweze kutupatia mafunzo haya kwa kuanza kwa mafunzo haya ya MEWEKA yatatusaidia sisi walimu kuweza kutumia ile elimu tutakayoipata kuweza kuwapatia wanafunzi wetu na jamii kwa ujumla.

Tunaishukuru Serikali tunaomba iendelee na mafunzo haya ”amesema Mwl. Bryson Rugemalila mshiriki wa mafunzo

Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini (MEWAKA) kwa Kanda ya Magharib yanaendela kufanyika Mikoa ya Kagera,Kigoma, Shinyanga na Tabora.

About the author

mzalendoeditor