Featured Kitaifa

SHEIKH RAJABU :’TUSIACHE KUYATENDA YALIYO MEMA,TUKUBALI KUHESABIWA’

Written by mzalendoeditor

Sheikh wa Mkoa wa Dodoma Alhaj Mustapha Rajabu Shabani akizungumza na kutoa nasaha kwa waumini wa dini ya Kiislamu waliohudhuria katika Swala ya Eid el Fitri iliyofanyika katika Msikiti wa Gaddafi jijini Dodoma

Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu waliohudhuria katika Swala ya Eid el Fitri iliyofanyika katika Msikiti wa Gaddafi jijini Dodoma

Sheikh wa Mkoa wa Dodoma Alhaj Mustafa Rajabu Shabani (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa dini ya Kiislamu Mkoa wa Dodoma

…………………………………………………

Na Bolgas Odilo -DODOMA.

WAUMINI wa Dini ya Kiislamu wameaswa kuendeleza kutenda yale yaliyo mema waliyokuwa wakiyatenda wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kama ilivyoagizwa na Mtume S.W.A .

Hayo yamesemwa na Sheikh wa Mkoa wa Dodoma Alhaj Mustapha Rajabu Shabani katika swala ya Eid iliyofanyika kimkoa kwenye msikiti wa Gaddaf jijini Dodoma.

Pia Sheikh Mustafa aliwataka waumini wa dini ya Kiislamu nchini kutopuuza zoezi za sense kwa kuwa ni muhimu na lina maslahi kwao na Taifa kwa ujumla katika kuleta maendeleo nchini.

“Kumekuwa na tabia ya waumini wengi kutenda matendo mazuri wakati wa mwezi wa Ramadhani tu baada ya hapo wanaendelea na matendo yasiyompendeza Allah.

“Niwaombe ndugu zangu, tuyaendeleze yale yote mazuri tuliyokuwa tukiyafanya kwenye mwezi mtukufu wa Ramadhani.    

“Tunaelekea katika kipindi muhimu cha sensaya watu na makazi, hii ni kwaajili ya maslahi yetu na kwa Taifa letu tukubali kuhesabiwa na tuwe tayari kutangaza sensa kwa wenzetu wengine.

“Tukijitokeza katrika zoezi hili itasaidia serikali kujua ina watu wangapi ili wanapopanga mipangilio yao ya bajeti waweze kuendana na kiwango cha watu waliokuwepo ili kusiwe na malalamiko miongoni mwetu,” alisema Sheikh Mustafa.

About the author

mzalendoeditor