Featured Michezo

YANGA YAZIDI KUPUNGUZWA KASI MBIO ZA UBINGWA

Written by mzalendoeditor

NA Alex Sonna

KLABU ya yanga imeendelea kupunguzwa kasi katika mbio za ubingwa mara baada ya kupata sare ya pili mfululizo kwa kutoka sare ya bila kufungana na wenyeji  Ruvu Shooting mchezo uliopigwa katika uwanja wa Lake Tanganyika Mkoani Kigoma.

Mechi hiyo ambayo ilikuwa ya aina yake licha ya Mshambuliaji hatari wa Yanga Fiston Mayele kugongesha mwamba mara mbili hakuweza kufunga kabisa kwenye mchezo huo ambao unakuwa wa pili kutokufunga mara baada ya kushindwa kutikisa nyavu kwenye mchezo uliopita.

Kwa matokeo hayo Yanga wamefikisha Pointi 56 huku ikibakiwa na mechi nane na kuendelea kukaa kileleni mwa ligi kuu NBC  ,Ruvu Shooting wamefikisha Pointi 22.

Ruvu Shooting watashuka dimbani Mei 8,2022 katika uwanja wa Benjamin Mkapa kwa kucheza na Simba yenye pointi 43 nafasi ya pili huku ikibakiwa na mechi 9 ligi kumalizika huku akiwa na tofauti ya pointi 13 na Yanga.

About the author

mzalendoeditor