KATIBU Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Eliamani Sedoyeka,akifungua kikao cha pamoja na waandishi wa habari wa Mkoa wa Dodoma leo Mei 5,2022 jijini Dodoma kuwajengea uwezo kuhusu Wiki ya Ubunifu Tanzania 2022 iliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO inayoambatana na Kilele cha Mashindano ya Kitaifa ya MAKISATU yanayotarajia kufanyika kufanyika Dodoma kuanzia Mei 15 hadi 20, 2022.
KATIBU Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Eliamani Sedoyeka,akifafanua jambo kwa washiriki (hawapo pichani) wakati wa kikao cha pamoja na waandishi wa habari wa Mkoa wa Dodoma leo Mei 5,2022 jijini Dodoma kuwajengea uwezo kuhusu Wiki ya Ubunifu Tanzania 2022 iliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO inayoambatana na Kilele cha Mashindano ya Kitaifa ya MAKISATU yanayotarajia kufanyika kufanyika Dodoma kuanzia Mei 15 hadi 20, 2022.
Mkurugenzi wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Maulilio Kipanyula,akizungumza wakati wa kikao cha pamoja na waandishi wa habari wa Mkoa wa Dodoma leo Mei 5,2022 jijini Dodoma kuwajengea uwezo kuhusu Wiki ya Ubunifu Tanzania 2022 iliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO inayoambatana na Kilele cha Mashindano ya Kitaifa ya MAKISATU yanayotarajia kufanyika kufanyika Dodoma kuanzia Mei 15 hadi 20, 2022.
Meneja wa Programu ya FUNGUO ya UNDP, Joseph Manirakiza,akieleza jambo kwa washiriki wakati wa kikao cha pamoja na waandishi wa habari wa Mkoa wa Dodoma leo Mei 5,2022 jijini Dodoma kuwajengea uwezo kuhusu Wiki ya Ubunifu Tanzania 2022 kilichoandaliwa na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO inayoambatana na Kilele cha Mashindano ya Kitaifa ya MAKISATU yanayotarajia kufanyika kufanyika Dodoma kuanzia Mei 15 hadi 20, 2022.
SEHEMU ya washiriki wakifatilia hotuba ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Eliamani Sedoyeka (hayupo pichani) wakati wa kikao cha pamoja na waandishi wa habari wa Mkoa wa Dodoma leo Mei 5,2022 jijini Dodoma kuwajengea uwezo kuhusu Wiki ya Ubunifu Tanzania 2022 kilichoandaliwa na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO inayoambatana na Kilele cha Mashindano ya Kitaifa ya MAKISATU yanayotarajia kufanyika kufanyika Dodoma kuanzia Mei 15 hadi 20, 2022.
Mwakilishi wa Waandishi Mkoa wa Dodoma ambaye ni Mwandishi wa Redio Uhuru FM,Sakina Abdulmasoud,akitoa neno la shukrani kwa niaba ya waandishi mara baada ya kikao cha pamoja na waandishi wa habari wa Mkoa wa Dodoma leo Mei 5,2022 jijini Dodoma kuwajengea uwezo kuhusu Wiki ya Ubunifu Tanzania 2022 kilichoandaliwa na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO inayoambatana na Kilele cha Mashindano ya Kitaifa ya MAKISATU yanayotarajia kufanyika kufanyika Dodoma kuanzia Mei 15 hadi 20, 2022.
KATIBU Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Eliamani Sedoyeka akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua kikao cha pamoja na waandishi wa habari wa Mkoa wa Dodoma leo Mei 5,2022 jijini Dodoma kuwajengea uwezo kuhusu Wiki ya Ubunifu Tanzania 2022 kilicoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO inayoambatana na Kilele cha Mashindano ya Kitaifa ya MAKISATU yanayotarajia kufanyika kufanyika Dodoma kuanzia Mei 15 hadi 20, 2022.
………………………………………..
Na Bolgas Odilo-DODOMA
KATIBU Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Eliamani Sedoyeka amesema katika bajeti ya mwaka 2022/23 Wizara imetenga fedha Shilingi bilioni 5.5 kwa ajili ya kuweka mazingira wezeshi ya kubuni, kuendeleza ubunifu pamoja na kujengea uwezo Taasisi na mbunifu mmoja mmoja.
Hayo ameyasema leo Mei 4,2022 Jijini Dodoma ,wakati kikao cha pamoja na waandishi wa habari wa Mkoa wa Dodoma kuwajengea uwezo kuhusu Wiki ya Ubunifu Tanzania 2022 iliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO inayoambatana na Kilele cha Mashindano ya Kitaifa ya MAKISATU yanayotarajia kufanyika kufanyika Dodoma kuanzia Mei 15 hadi 20, 2022.
Amesema katika bajeti ya Mwaka 2021/22 inayoishia Juni 30 mwaka huu, kiasi cha Sh. bilioni moja kilitengwa kwa ajili ya kuendeleza wabunifu nchini ambapo tayari wengine wameshanufaika.
Aidha, amesema mpaka sasa Serikali imeshatumia takribani Sh Bilioni 2.3 kuendeleza takribani wabunifu 200 walioibuliwa na kutambuliwa na ubunifu wao kuingizwa kwenye kanzidata ya nchi.
“Wajibu wa Wizara pamoja na majukumu mengine ni kuibua, kutambua na kuendeleza ubunifu na teknolojia zinazozalishwa nchini na kuhamasisha matumizi yake katika kutatua changamoto za kiuchumi na kijamii,” amesema Prof.Sedoyeka.
Ameongeza kuwa sayansi na teknolojia ni muhimu duniani kote katika kuchochea kasi ya kimaendeleo, kiuchumi na kijamii na ndio maana Wizara imekuwa ikiwaibua na kuwandeleza wabunifu hao ili kuongeza tija katika uzalishaji wa bidhaa na hata utoaji huduma.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Maulilio Kipanyula amesema mwaka huu jumla ya wabunifu 862 kutoka makundi ya shule za Msingi na Sekondari, Vyuo vya Ufundi, Vyuo vya Ufundi wa Kati, Mfumo usio rasmi, Taasisi za Utafiti na Vyuo Vikuu wamewasilisha ubunifu wao kwa ajili ya kushindanishwa.
Ameongeza kuwa Wizara imeendelea kuandaa mazingira wezeshi ili wabunifu waweze kuonekana pamoja na ubunifu wao kuendelezwa kwa kushirikiana na wadau ili ubunifu uweze kufikia biashara.
Awali Meneja wa Programu ya FUNGUO ya UNDP, Joseph Manirakiza amesema wamekuwa wakishirikiana na Wizara katika kuwaendeleza wabunifu, kutoa msaada wa kitaalamu kwa wabunifu hao kupitia kumbi za atamizi lakini pia kushirikiana na Serikali kuweka mazingira rafiki ya wabunifu katika kuendesha biashara.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Waandishi Mkoa wa Dodoma ambaye ni Mwandishi wa Redio Uhuru,Sakina Abdulmasoud ameishukuru Wizara hiyo kwa kuandaa semina ambayo imewasaidia kupata uelewa kuhusu mambo ya ubunifu.
Sakina ambaye ni Balozi wa Mazingira,amewataka wabunifu kubuni teknolojia ambazo ni rafiki katika masuala ya mazingira huku akisema wataendelea kufanya kazi pamoja na Wizara hiyo.
”Nakipongeza kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Wizara hiyo kwa kuonesha ushirikiano mkubwa kwa waandishi hivyo wataunganisha nguvu zao kama waandishi ili kuielimisha jamii juu ya bunifu’amesema Balozi Sakina
Wiki ya Ubunifu Tanzania kwa mwaka huu ina kauli mbiu “Ubunifu kwa Maendeleo Endelevu” na inashirikisha wabunifu 86 ambao wameshindanishwa kutoka kwa wabunifu 862 waliowasilisha bunifu zao.