Featured Kitaifa

WAZIRI UMMY :’TUTASHIRIKIANA NA WADAU KUWA NA ENEO LA WATOTO KUSHEHEREKEA SIKUKUU JIJINI TANGA’

Written by mzalendoeditor


WAZIRI
wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akizungumza
jambo mara baada ya kutoka Msikiti wa Ijumaa kulipofanyika swala ya Eid
El Fitri Kimkoa


WAZIRI
wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akitoa kwenye
msikiti mkuu wa Ijumaa Jijini Tanga mara baada ya swala ya Eid El Fitri


WAUMINI wa dini ya Kiislamu Jijini Tanga wakiswali swala ya Eid El Fitri katika Msikiti Ijumaa Jijini Tanga leo

WAZIRI
wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katika akiwa
kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika swala ya Eid El Fitri
WAZIRI wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katika
akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika swala ya Eid El
FitriWAZIRI wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katika
akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika swala ya Eid El
Fitri

WAZIRI
wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kushoto akiwa na
nje ya msikiti wa Ijumaa mara baada ya kumalizika swala ya Eid El Fitri
leo

NA MWANDISHI WETU,TANGA.

WAZIRI wa
Afya na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu leo  ameshiriki katika
swala ya Eid El Fitri kwenye Msikiti wa Ijumaa Jijini humo huku akihaidi
kushirikiana na wadau kuhakikisha wanakuwa na eneo la watoto kusheherekea
sikukuu.

Ummy
aliyasema hayo mara baada ya kumalizika kwa swala hiyo iliyohudhuriwa na
waumini kutoka maeneo mbalimbali Jijini humo ambapo alisema kwamba wanafahamu
Jiji hilo bado halina sehemu kuchezea watoto hivyo atalifanyia kazi.

Alisema
kwamba eneo hilo ambalo wanatarajia kuhakikisha linakuwepo kwenye Jiji hilo
litawezesha wazazi kwenda kusheherekea na watoto sikukuu na hilo atakwenda
kuona namna ya kulifanyia kazi.

“Tunafahamu Jiji
la Tanga bado halina sehemu ya kuchezea watoto kwa hiyo tutalifanyia kazi kwa
kushirikiana na wadau kuhakikisha kuna kuwa na eneo kubwa na nzuri ambayo mzazi
atakwenda kusheherehea na watoto sikukuu”Alisema

“Lakini pia
katika sikukuu hii niwatakie kilalaheri wananchi wa Jimbo la Tanga  na niwashukuru kwa heshima kubwa ambayo
mmeendelea kunipa tutaendelea kushirikiana”Alisema

Aidha pia
Waziri Ummy aliwataka wakazi wa Tanga mjini heri ya sikuuu ya Eid El Fitri huku
akimuomba Mwenyezi Mungu azikubali funga zao na azipokee dua zilizofanyika
kipindi cha mwezi wa ramadhani.

 

Waziri huyo
aliwataka wananchi kuendelea kutenda mema kupendana na kushirikiana na kufanya
ibada ya kujinyenyekeza kwa mungu na wasichoke kumuomba mwenyezi mungu.

 

Hata hivyo
aliwataka watoto washeherekee vizuri sikukuu isifike usiku huku akiwataka wanapotoka
kwenda kutembea watoto waende na watu wazima ambao watawasimamia kwa sababu kwenye
kipindi cha idd kuna watu wanaweza kufanya mambo maovu.

About the author

mzalendoeditor