Katibu Mkuu wa Chama cha UDP Samia Rashid akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea na kukagua ujenzi wa Ofisi mbali mbali za Wizara zilizopo Mji wa Kiserikali Mtumba pamoja na ujenzi wa Soko la Kisasa la Wamachinga lililopo Bahi Road jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Watu Wenye Ulemavu Dodoma Amina Issa,akiiomba Serikali kuweka miundombinu rafiki kwa Watu wenye Ulemavu kwenye majengo yanayojengwa baada ya kutembelea Mji wa Kiserikali Mtumba pamoja na ujenzi wa Soko la Kisasa la Wamachinga lililopo Bahi Road jijini Dodoma.
Muonekano wa Mji wa Kiserikali Mtumba Jijini Dodoma ujenzi ukiwa bado unaendelea
Muonekano wa ndani wa soko la wamachinga jijini Dodoma
Jumuiya ya Wanawake wa Vyama vya Siasa wakiendelea na ukaguzi pamoja na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Soko la Wamachinga jijini Dodoma
Jumuiya ya Wanawake wa Vyama vya Siasa wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyeji wao Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka mara baada ya ziara ya kutembelea na kukagua ujenzi wa Ofisi mbali mbali za Wizara zilizopo Mji wa Kiserikali Mtumba pamoja na ujenzi wa Soko la Kisasa la Wamachinga lililopo Bahi Road jijini Dodoma.
……………………………………..
NaBolgas Odilo-Dodoma.
JUMUIYA ya Wanawake Viongozi wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania (T-WCP/ULINGO) wamepongeza juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika kulipeleka Taifa kwenye maendeleo zaidi kwa vitendo.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Katibu Mkuu wa Chama UDP, Bi.Samia Rashid,amempongeza Rais Samia kwa kuendelea kusimamia maendeleo ya nchi pamoja na kuwajaliwa watanzania wote kwa ujumla katika kuleta maendeleo ya nchi.
Miradi iliyotembelewa na Jumuiya hiyo ni ujenzi wa Ofisi mbali mbali za Wizara zilizopo Mji wa Kiserikali Mtumba jijini Dodoma pamoja na ujenzi wa Soko la Kisasa la Wamachinga lililopo Bahi Road.
“Tunampongeza Rais Samia na tunamtambua kama mfanyakazi bora kwa namna ambavyo anafanya kazi kubwa kwenye nchi yetu.
“Hii inaonesha kwamba vitu alivyoahidi kuwafanyia Watanzania na kuwafikisha kwenye maendeleo yanaendelea kutekelezwa kwa vitendo,”alisema Bi. Rashid.
Lakini pia aliongeza kwa kusema. “Serikali imefanya jukumu lake na sisi kama Watanzania kwenye haya maendeleo na miradi ambayo inatekelezwa tunajukumu la kuilinda kwa namna yeyote ile,”
Kwa upande wake Katibu wa Jumuiya ya Watu wenye Ulemavu Dodoma Amina Issa,amesema kuwa wanampongeza Rais Samia kwa kazi anazozifanya katika kuleta maendeleo nchini pamoja na kumshukuru kwa kuwapa nafasi za uongozi watu wenye ulemavu,
“Tunampongeza Rais Samia kwa kazi kubwa anazoendelea kuzifanya, asisahau kuweka miundombinu rafiki kwenye majengo haya anayoendelea kuyajenga.
“Pia tunamshukuru kwa kuwapa nafasi za uongozi watu wenye ulemavu na wameonesha mfano mkubwa kwenye uchapaji kazi wao na kweli tunaweza,” alisema Amina.