Featured Kitaifa

WANAWAKE NA VIJANA WALIOPO KATIKA SEKTA YA KILIMO BIASHARA WATAKIWA KUWA MABALOZI WAZURI KATIKA KUTOA ELIMU.

Written by mzalendoeditor

Naibu Waziri wa Mambo ya NdanI ya Nchi, Jumanne Sagini ambaye pia ni Mgeni Rasmi wa Mdahalo wa Kukuza Uwekezaji wa Wanawake na Vijana katika Sekta ya Kilimo Biashara akizungumza na wanawake na vijana walioalikwa kwenye mdahalo huo uliofanyika leo April 29,jijini Dodoma.
Naibu Waziri Sagini aliyemwakilisha Niabu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe kwenye ufunguzi wa Mdahalo huo amewataka wanawake na vijana katika sekta ya Kilimo Biashara kuwa mabalozi wazuri katika kutoa elimu na uelewa wa fursa, sera, kanuni na miongozo ya Serikali katika kukuza na kuendesha biashara.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa AMDT, Charles Ogutu (katikati) pamoja na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda-Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Christopher Mramba baada ya kufungua Mdahalo wa Kukuza Uwekezaji wa Wanawake na Vijana katika Sekta ya Kilimo Biashara uliofanyika Jijini Dodoma, leo Aprili 29,2022.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini ambaye pia ni Mgeni Rasmi wa Mdahalo wa Kukuza Uwekezaji wa Wanawake na Vijana katika Sekta ya Kilimo Biashara akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Wanawake na Vijana waliohudhuria katika mdahalo huo uliofanyika Jijini Dodoma, leo Aprili 29,2022.

About the author

mzalendoeditor