Featured Kitaifa

RAIS DK.MWINYI AHUDHURIA MAZIKO YA MAREHEMU TALIB HAJI JECHA NA MAREHEMU MWANAIDI KASSIM ALI MTEGANI MAKUNDUCHI MKOA WA KUSINI UNGUJA

Written by mzalendoeditor

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Sheikh.Abdalla Haji Laka, baada ya kumaliza kwa sala maiti ya Marehemu Talib Haji Jecha Baba Mzazi wa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Dkt.Mwinyi Talib Haji na Marehemu Mwanaidi Kassim Ali, Dada wa Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar Mhe.Rahma Kassim Ali, iliyofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Mtegani Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja leo 29-4-2022,baada ya kumalizika kwa Sala ya Ijumaa.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Sheikh Said Hamdu baada ya kumalizika kwa maziko ya Marehemu Talib Haji Jecha na Marehemu Mwanaidi Kassim Ali, yaliofanyika katika Kijiji cha Mtegani Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja na (kulia kwa Rais ) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Alhaj Othman Masoud Othman na (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar. Mhe.Haroun Ali Suleiman.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Mkuu wac Mkoa wa Kusini Unguja Mhe.Rashid Hadidi Rashid, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Dkt.Mwinyi Talib Haji, alipowasili katika Msikiti wa Ijumaa Mtegani Makunduchi Unguja kuhudhuria maziko ya Baba Mzazi wa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, yaliofanyika katika Kijiji cha Mtegani.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikosomwa na Imamu wa Msikiti wa Ijumaa Mtegani Makunduchi Sheikh. Abdalla Haji Laka baada ya kumalizika kwa Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika msikiti huo na (kulia kwa Rais) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.Alhaj Othman Masoud Othman na (kushoto kwa Rais) Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.Dkt.Mwinyi Talib Haji na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla, wakiitikia dua.

WAUMINI wa Dini ya Kiislam wakiitikia dua baada ya kumalizika kwa Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Mtegani Makunduchi Unguja.(Picha na Ikulu)

About the author

mzalendoeditor