Featured Kimataifa

MATUKIO KATIKA PICHA:MAKAMU WA RAIS AKISHIRIKI KUAGWA KWA MWAI KIBAKI KENYA

Written by mzalendoeditor

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango leo amemuwakilisha Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Mazishi ya kitaifa ya  aliyekuwa Rais wa Tatu wa Jamhuri ya Kenya ,Hayati Emilio  Mwai Kibaki. Ibada ya kumuaga Hayati Mwai Kibaki imefanyika katika Uwanja wa Nyayo uliopo Nairobi nchini Kenya na kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta. 

Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa mbalimbali, wawakilishi wa taasisi za kitaifa na kimataifa pamoja na mabalozi, wananchi wa Kenya na nchi jirani wamehudhuria kuagwa kwa Hayati Mwai Kibaki.

…………………………………….

Katika tukio hilo, Makamu wa Rais ameongozana na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM – Bara) Komredi Abdulrahman Kinana pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Mbarouk.

Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa mbalimbali, wawakilishi wa taasisi za kitaifa na kimataifa pamoja na mabalozi, wananchi wa Kenya na nchi jirani wamehudhuria kuagwa kwa Hayati Mwai Kibaki.

About the author

mzalendoeditor