Featured Kitaifa

TAASISI YA UONGOZI YATAKIWA KUFANYA TAFITI KWA VIONGOZI 

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na watumishi wa Taasisi wa Uongozi jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao. Kulia kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Bw. Kadari Singo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye kikao kazi na watumishi wa Taasisi wa Uongozi jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Bw. Kadari Singo akielezea majukumu ya ofisi yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama wakati wa ziara ya kikazi ya Mhe. Jenista ya kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa Taasisi ya Uongozi.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Bw. Kadari Singo akipokea malekezo toka kwa kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama wakati wa ziara ya kikazi ya Mhe. Jenista ya kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa Taasisi ya Uongozi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Taasisi ya Uongozi baada ya kikao kazi chake na watumishi hao kilicholenga kuhimiza uwajibikaji.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Mshauri Mkuu-Ushirikiano, Bw. Konsta Heikkila baada ya kikao kazi chake na watumishi wa Taasisi ya Uongozi kilicholenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa taasisi hiyo.

…………………………………………….

Na. Veronica Mwafisi-Dar es Salaam

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama, ameilekeza Taasisi ya Uongozi kufanya tafiti za kina kwa viongozi ili kubaini mapungufu waliyonayo kwa lengo la kuandaa programu zitakazosaidia kutoa mafunzo kulingana na mapungufu yatakayobainishwa hatimaye kuwa na viongozi bora kwa ustawi wa maendeleo ya taifa.

Mhe. Jenista ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kikazi katika Taasisi ya Uongozi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa taasisi hiyo.

 “Tunataka mtutizame sisi viongozi ili muweze kubaini mapungufu tuliyonayo na kututengenezea programu zitakazosaidia kuboresha mapungufu yetu, kama Taasisi ya Uongozi tunatakiwa tufikiri kwa kina kuona ni namna gani tunaweza kusaidia katika hili,” Mhe. Jenista amesisitiza.

Mhe. Jenista amesema ari aliyonayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa nchi yake ni kubwa sana na ndio maana amekuwa akisisitiza sana suala la kufanya tathmini na ufuatiliaji hivyo, ni vizuri kujua kinachohitajika na kutumia tathmini zilizopo ili zisaidie kuboresha kwa maendeleo ya taifa.

Mhe. Jenista ameongeza kuwa viongozi wanahitaji mafunzo ya kina, kwani mfumo wa kufikiri unaweza ukawa ni ule ule tangu uhuru lakini ni vizuri wakapata mafunzo ili kuongeza vitu vipya katika uelewa wa mambo mbalimbali.

Mhe. Jenista amesema ni vema Taasisi ya Uongozi iangalie majukumu shirikishi yanayoambatana na malengo makuu ya taasisi hiyo na kufikiri zaidi kwa kuitazama nchi na kuangalia maeneo yanayoweza kusaidia kufanya mageuzi makubwa kwa ustawi wa maendeleo ya taifa.

Aidha, Mhe. Jenista amewataka watumishi wa taasisi hiyo kujifunza kutoka nchi nyingine mambo mazuri waliyo nayo ili kupata ujuzi zaidi kwani taasisi inayofanana na ya kwao zipo kwenye mataifa mengi ila zinatofautiana kwenye miundo na mifumo, hivyo kujifunza kutoka kwao kutasaidia kupata ujuzi zaidi kwa maendeleo ya nchi yetu.

About the author

mzalendoeditor