Featured Kitaifa

RAIS SAMIA ATOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 3,826

Written by mzalendoeditor

Tarehe 26 Aprili, 2022 Huwa tunaadhimisha Miaka 58 ya Muungano wa Tanzania. Hili ni tukio muhimu na la kihistoria kwa Taifa letu. Katika maadhimisho hayo, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya Ibara ya 45(1)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa msamaha kwa wafungwa 3,826. 

  1. 2. 

Kwa masharti yafuatayo: 

(i) 

Wafungwa wote wapunguziwe robo (1/4) ya vifungo vyao baada ya punguzo la kawaida la moja ya tatu (1/3) linalotolewa chini ya Kifungu cha 49 (1) cha Sheria ya Magereza, Sura ya 58. Wafungwa hao sharti wawe wametumikia robo (1/4) ya vifungo vyao na wawe wameingia gerezani kabla ya tarehe 26 Februari, 2022 isipokuwa wafungwa walioorodheshwa katika sharti la 2(i–ii); 

(ii) Wafungwa wagonjwa wenye magonjwa ya kudumu ambao wametumikia 

robo (1/4) ya vifungo vyao na wapo kwenye Terminal Stage, ugonjwa huo uthibitishwe na jopo la waganga chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya; 

(iii) Wafungwa wazee wenye umri wa miaka sabini (70) au zaidi ambao 

wametumikia robo (14) ya vifungo vyao. Umri huo uthibitishwe na jopo la 

waganga chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya; 

(iv) Wafungwa wa kike walioingia gerezani wakiwa na watoto wanaonyonya, 

wasionyonya na wajawazito ambao wametumikia robo (1/4) ya vifungo 

vyao; (V) Wafungwa wenye ulemavu wa mwili na akili (physical disability and 

mental disability) ambao wametumikia robo (1/4) ya vifungo vyao. Ulemavu huo uthibitishwe na jopo la waganga chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya; 

(vi) Wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kuwekwa kizuizini (Under 

President’s Pleasure) ambao wamekaa gerezani kuanzia miaka kumi (10) na kuendelea; 

(vii) Wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kifo ambao wamekaa gerezani 

kuanzia miaka thelathini (30) na kuendelea; 

(viii) Wafungwa wanaotumikia kifungo cha maisha gerezani ambao wamekaa 

gerezani kuanzia miaka ishirini (20) na kuendelea; 

(ix) Wafungwa wanaotumikia adhabu kwa makosa ya kujaribu kuua (Attempt 

to Murder) ambao wamekaa gerezani kuanzia miaka kumi (10) na kuendelea; 

(x) Wafungwa wanaotumikia adhabu kwa makosa ya kujaribu kujiua 

(Attempt Suicide) ambao wamekaa gerezani kuanzia miaka kumi (10) na 

kuendelea; 

(xi) Wafungwa wanaotumikia adhabu kwa makosa ya kuua watoto wachanga 

(Infanticide) ambao wamekaa gerezani kuanzia miaka kumi na tano (15) na kuendelea; 

(xii) Wafungwa wanaotumikia adhabu kwa makosa ya uhujumu uchumi 

ambao wamekaa gerezani kuanzia miaka ishirini (20) na kuendelea; 

(xiii) Wafungwa wanaotumikia adhabu kwa makosa ya matumizi mabaya ya 

madaraka yao ambao wamekaa gerezani kuanzia miaka mitano (05) na 

kuendelea; 

(xiv) Wafungwa wanaotumikia adhabu kwa makosa ya utakatishaji wa fedha 

ambao wamekaa gerezani kuanzia miaka ishirini (20) na kuendelea; 

(xv) Wafungwa wanaotumikia adhabu kwa makosa ya rushwa ambao 

wamekaa gerezani kuanzia miaka kumi (10) na kuendelea; 

(xvi) Wafungwa wanaotumikia adhabu kwa makosa ya usafirishaji wa madawa 

ya kulevya ambao wamekaa gerezani kuanzia miaka ishirini (20) na kuendelea; 

(xvii) Wafungwa wanaotumikia adhabu kwa makosa ya utekaji au wizi wa 

watoto ambao wamekaa gerezani kuanzia miaka kumi (10) na kuendelea; na 

(xviii) Wafungwa wanaotumikia adhabu kwa makosa ya wizi au ubadhirifu wa 

fedha na mali za umma ambao wamekaa gerezani kuanzia miaka kumi na tano (15) na kuendelea. 

  1. 3. 

Aidha, msamaha huu usiwahusishe wafungwa wafuatao: 

(i) 

(ii) 

Wafungwa wa madeni; na Wafungwa wanaotumikia kifungo chini ya Sheria ya Bodi za Parole, Sura ya 400 Sheria ya Huduma kwa Jamii (Sura ya 291) na Kanuni za Kifungo cha Nje {The Prisons (Extra Mural Penal Employment) Regulations}, 1968. 

About the author

mzalendoeditor