KIKOSI cha Simba kimerejea Dar es Salaam baada ya kutolewa na wenyeji, Orlando Pirates katika Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa penalti 4-3 Jijini Johannesburg, Afrika Kusini kufuatia sare ya jumla ya 1-1, kila timu ikishinda 1-0 nyumbani.
Moja kwa moja Simba inaingia kambini kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya mahasimu, Yanga Jumamosi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.