Featured Kitaifa

WATOTO NA VIJANA WATAKIWA KUISHI KATIKA MAADILI MEMA

Written by mzalendoeditor

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Badru Abdulnuru akizungumza katika Iftar iliyoandaliwa na Kituo cha Redio Cha CFM jijini Dodoma ajili ya Watoto na vijana wanaiishi katika mazingira magumu, Mkurugrenzi huyo alimwakilisha Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Mwanaidi Ali Khamis.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Badru Abdulnuru (kushoto) akijadiliana jambo na Mwakilishi wa Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Sheikh Ahmed Said (kulia) wakati wa Iftar iliyoandaliwa na Kituo cha Redio CFM jijini Dodoma kwa ajili ya Watoto na vijana waishio katika mazingira magumu 

Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Lucas Mbise akizungumza katika Iftar iliyoandaliwa na Kituo cha Redio Cha CFM jijini Dodoma kwa ajili ya Watoto na vijana waishio katika mazingira magumu.

Mwakilishi wa Sheikh wa Mkoa wa Dodoma Sheikh Ahmed Said akizungumza wakati wa Iftar iliyoandaliwa na kituo cha Redio Cha CFM jijini Dodoma kwa ajili ya Watoto na vijana waishio katika mazingira magumu

Baadhi ya Watoto waliojumuika katika Iftar iliyoandaliwa kwajili ya kufuturisha Watoto na vijana waishio katika mazingira magumu iliyoandaliwa na Kituo cha Redio Cha CFM jijini Dodoma. Halfa hiyo iliudhuriwa na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Jinsia kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Badru Abdulnuru akimwakilisha Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Mwanaidi Ali Khamis.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Badru Abdulnuru katika picha ya pamoja na baadhi ya walezi wa Watoto na vijana wanaoishi katika Mazingira magumu mara baada ya Iftar iliyoandaliwa na Kituo cha Redio Cha CFM jijini Dodoma kwa ajili ya Watoto na vijana hao 

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Badru Abdulnuru akimlisha mtoto keki mara  mara baada ya Iftar iliyoandaliwa na Kituo cha Redio Cha CFM jijini Dodoma.

Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WMJJWM

……………………………………………..

Na WMJJWM- Dodoma

Watoto na Viijana nchini wameaswa kuachana na vitendo viovu na kuwa na tabia zitakazowezesha kuharibu maisha yao na kushindwa kutimiza ndoto zao katika maisha.

Rai hiyo imetolewa Jijini Dodoma tarehe 23, Aprili 2022 na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Jinsia kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Badru Abdulnuru alipokuwa akimwakilisha Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mwanaidi Ali Khamis katika iftar iliyoandaliwa na Kituo cha Redio cha CFM kwaajili ya Watoto na vijana wanaoishi katika mazingira hatarishi na magumu.

Akizungumza katika Iftar hiyo Bw. Badru alisema kundi la Watoto na vijana linapaswa kuishi katika maadili mema kama inavyofundishwa na dini, wazazi na walezi ili waweze kufikia ndoto zao kwani ndio wazazi na Viongozi wajao hivyo ni vyema kujua katika maadili yakayosaidia kuwa na taifa imara.

Ameongeza kuwa Serikali imeendelea kuhakikisha inaweka misingi mbalimbali itakayosaidia Watoto na Vijana kuepukana na changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo maambukizi ya virusi ya VVU na UKIMWI ikiwemo Ajenda ya Kitaifa ya Kuwekeza katika Afya na Maendeleo ya Vijana Balehe (2021/2022 – 2024/20225) .

Amesisitiza kuwa mtoto au kijana unayeishi katika Mazingira magumu sio kuwa umekosea sana katika ulimwengu bali Mwenyezi Mungu anajua maisha ya Watoto na vijana hao hivyo wataendelea kuungana na Serikali na wadau wengine kuhakikisha wanatoanhuduma kwa watoto na vijana wanaoishi katika Mazingira magumu ili waweze kupata huduma hizo.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Lucas Mbise alisema Wilaya hiyo imekuwa ikishirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha Watoto na vijana wanaoishi kwenye Mazingira Hatarishi wanapata huduma na misaada mbalimbali ya kijamii ili waweze kuishi angalau katika mazingira yatakayowapa faraja na matumaini.

“Niwasihi watoto na vijana mliopo hapa kwenye hii Iftar msikate tamaa kwa maana nafasi uliyonayo hapa kwa uzima na uhai tuendelee kumuomba Mwenyezi Mungu atujalie uzima na kufikia katika ndoto zenu mlizonazo” alisema Mbise

Naye Mkurugenzi wa Biashara na Ubunifu kutoka CFM Nickson George alisema lengo la Iftar hiyo ni kujumuika na Watoto na vijana wanaoishi katika Mazingira Hatarishi kwa kuwapa faraja katika kipindi hiki cha Mfungo wa Mwezi mtukufu wa Ramadhan na Watoto na Vijana hao wametokea katika Vituo vinne vya kuelekea Watoto na Vijana vilivyopo jijini Dodoma.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Sheikh wa Mkoa wa Dodoma Sheikh Ahmed Said alisema suala walilofanya Kituo cha Redio Cha CFM kuwa ni jambo kubwa na jema hasa katika kipindi hiki cha Mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Nao baadhi ya Watoto na vijana wanaoishi katika Mazingira magumu kutoka katika Vituo vinne jijini Dodoma wameiomba Serikali na wadau mbalimbali kuendelea kuwaangalia kwa jicho la pekee Watoto na vijana wanaoishi katika Mazingira magumu nchini hasa kwa Mkoa wa Dodoma.

Aidha wamewashukuru walezi kutoka katika vituo mbalimbali vinavyolea Watoto na vijana hao kwa kuwapa Malezi na mapenzi ila bado wanaohitaji msaada kutoka kwa Serikali na wadau ili kuendelea kuendeleza ndoto za Watoto na vijana hao kujiendeleza kimaisha.

About the author

mzalendoeditor